NIKKI AFUNGUKA ALIVYOSOMESHWA CHUO NA RUGE

Nickson Simon

IKIWA imepita wiki moja tangu afariki dunia Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba, staa wa Bongo Fleva, Nickson Simon amefunguka kuwa alisomeshwa naye elimu ya chuo kikuu (UDSM).  

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Nikki ambaye ni memba wa Kundi la Weusi alisema kuwa, wakati anasoma Shahada ya Uzamivu (PHD) alikutana na Ruge na kumuulizia elimu yake.

 

“Nilikutana naye akaniuliza hivi unasoma nini chuo kikuu nikamwambia Shahada ya Uzamivu basi akasema kuwa anapenda watu wanaojituma katika kusoma nikaachana naye.

 

“Siku mbili mbele nashangaa wanakuja watu na kuniambia kuwa wametumwa na Ruge kwa ajili ya kunilipia ada yote,” alisema Nikki.

Toa comment