The House of Favourite Newspapers

PRINCE STATIONERY WAONGEZA OFA PUNGUZO LA VIFAA VYA SHULE

  WAUZAJI bingwa wa vifaa vya maofisini na shuleni, kwa bei za jumla na rejareja, Prince Stationery ambao Januari mwaka huu walitangaza ofa kubwa kwa wazazi na wanafunzi wanaohitaji vifaa vya mashuleni kwa ajili ya muhula mpya wa masomo, sasa wameongeza muda wa ofa hiyo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Meneja Mkuu wa Prince Stationery, Abdul Aziz Khatib, amesema wanatambua kwamba uhitaji wa vifaa vya shule si kwa mwezi wa Januari na Februari pekee, kwa hiyo wameamua kuongeza muda wa ofa ili kuwapa nafasi zaidi wazazi kuwanunulia watoto wao vifaa vya shule kwa bei nafuu.

“Vifaa vinavyopatikana kwenye maduka yetu ni pamoja na madaftari ya kawaida, makubwa na madogo, counter books, mathematical sets (mikebe), kalamu za aina zote, rangi, vifutio (eraser), calculator, nguo za michezo kwa wanafunzi pamoja na vifaa vingine vingi,” alisema Abdul Aziz.

Akaongeza kwamba, mbali na kutoa huduma kwenye maduka yao mawili yaliyopo Kariakoo, Plot Number 12, Block 4, Mtaa wa Lindi jirani na msikiti, na duka lingine lililopo Mtaa wa Kongo, wanao uwezo wa kuwahudumia wateja hata waliopo mikoani, kwa kuwafikishia mzigo mpaka mlangoni kwa gharama nafuu sana.

“Kwa wateja wa mikoani, tunawatumia mzigo mpaka mahali popote walipo, wao wanalipia kiasi kidogo tu kwa ajili ya usafiri na wao ndiyo wanaochagua mzigo utumwe kwa njia ipi. Uzuri ni kwamba bidhaa zetu ni za kiwango cha juu na zina ubora mkubwa kwa hiyo mteja ataridhika kwa asilimia mia moja mahali popote alipo,” alisema Abdul Aziz.

 

Mbali na huduma za vifaa vya mashuleni, Prince Stationery pia wanauza mapambo ya ndani, vifaa vya maofisini, michezo ya watoto na vifaa vya maharusi kwa bei poa kabisa.

Wasiliana nao kwa namba za simu 0774 880 082 kwa Duka la Mtaa wa Congo na 0686 942 978 kwa Duka la Mtaa wa Lindi, au unaweza kuwatembelea kwenye mitandao ya kijamii;

Instagram: prince_stationery_tz

Facebook: prince stationery

Twitter: prince_ssb_tz

Email: [email protected].

Waweza pia kuwatembelea kwenye mtandao wao kwa anuani ya www.princesecretarial.co.tz

Na Mwandishi Wetu

===USIPITWE! Duka Linalouza Magari ya Kifahari ya Watoto, Lazua Gumzo Kariakoo==

Comments are closed.