The House of Favourite Newspapers

Nilianza Kupika Chakula cha Kienyeji, Hawakunielewa, Leo ni Shujaa!

0

WAKATI  naanzisha wazo la kutoa huduma ya vyakula vya vya asili watu  wengi walinidhihaki kwa kupika vyakula vya kienyeji  na hawakunielewa. Hata hivyo, leo hii mimi ni shujaa wa aina yangu kwani wanakuja watu wa mataifa yote duniani makubwa kwa madogo kula vyakula vyangu.

 

Historia hii ilianzia mbali mnamo miaka ya tisini ambapo hapakuwa na mgahawa (restaurant) uliokuwa unapika vyakula kama wali, ugali, ndizi, samaki n.k. 

Wakati huo ukienda mjini maeneo ya Posta au Kariakoo ndipo utakuta chips samaki aina ya kibua au changu  na chakula kilikuwa kinapatikana kuanzia saa sita mchana mpaka saa tisa tu, baada ya hapo ilikuwa huwezi kupata.

 

Watu wengi wengi makazini walikuwa na mazoea ya kurudi nyumbani kwenda kula. Kwenye mabaa mengi mtu akienda, ilikuwa ni kwa ajili ya kula kongoro, ulimi, mkia, mishikaki na mbuzi-choma tu au supu ya mbuzi.  Hapakuwepo kuku wa kienyeji na maji ya kunywa, mengi yalikuwa ya kuchemsha wala si ya chupa.

 

Hata juisi ilikuwa inapatikana tu kwa wafanyabiashara wa Kipemba au Wasomali. Waswahili hatukuwa na wazo la kutengeneza juisi majumbani kwetu. Wazo hili nililifanyia utafiti kwa mda wa miaka mitatu nikagundua kwamba Watanzania tuna tatizo la kutofanya uthubutu.

 

Niliamua kuanzisha biashara ya vyakula vya kienyeji na baadaye vyakula vya kigeni kama burger na  pizza, nikiwa nimeanua kutoa huduma kwa watu muda wowote ule.

Nakumbuka siku moja nilikutana na vijana wanne akiwemo Joseph Kusaga ambapo katika mazungumzo yetu liliibuka wazo  kuanzisha kituo cha radio ambacho leo hii ni Clouds Group ambayo ni brand kubwa nchini.

 

Wakati huo nilikuwa sijafungua Break Point (BP), nikiwa na sehemu yangu eneo la Igongwe Bar Mwenge ambayo niliachiwa na kaka yangu, Dr Shariff Maajar mume wa Balozi Mwanaidi Maajar.

 

Wateja wangu wakubwa walikuwa ni pamoja na Prof. Luoga, Gavana wa Benki Kuu (B.O.T) ambaye naye alikuja kuwa mwasisi wa jina Brake Point, marehemu John Ngogo (Ruaha Across),  marehemu Prof Setty Chachage (UDSM), Alison Mtembei (REPOA), Dr Mpango Waziri wa Fedha, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki,  Charles Hilary wa Azam TV,  Dr Ayubu Rioba wa TBC, Deo Rweyunga ITV, Francis Nanai wa Mwananchi Communication na Mheshimiwa  Eric Shigongo,  kwa uchache, na wafanyakazi wote wa Brake Point wa sasa na zamani walioifanya BP iinuke na kupata umaarufu.

Ubunifu uliendelea kwa muda wa miaka 18 tukaifanya BP kuwa maarufu katika sayari hii.

 

Mimi na wenzangu tulikuwa tukienda kwa mzee mmoja mjini aliyekuwa anaitwa Makange, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam,  ambapo tulikuwa tunakula kuku tuliyekuwa tunamtoweza  kwa ndimu.

 

Hivyo nikaona katika mapishi yangu nianzishe chakula kinachoitwa Makange  ili  nimuenzi mzee huyo.  Hili liliwezekana baada ya mimi  kuwachukua pia vijana wake (wapishi)  na kuwahamishia kwangu.  Hivyo chakula hicho kikaitwa Makange.

Nikaanzisha utaratibu wa wahudumu kuwalipa kwa vivutio (incentive) huduma zetu ili kila mtu akifika BP lazima azitofautishe na wengine. Ugali wa mhogo, mtama, ulezi, kamongo, kitoga, kibambara, Brenda Fassie, Redsnapper Soup, Dot.com, Mbuzi Unyunu, chukuchuku sato/kuku wa kienyeji, kichuri, Masai Mara, Local, Obama Spice na Dar – Dom vikawa vyakulavilivyotupaisha mjini.

 

Hakika biashara ni mchezo mzuri kama Waingereza wanavyosema kwamba: Business is a Nice Joke, Nilichojifunza kwenye biashara ni kwamba hakuna umri wa binadamu utakaodumu ukalinganisha na Brand kama itasimamiwa vizuri.

 

Miaka 21 ya Brake Point na ufunguzi wa tawi jipya la Brake Point Kijijini ni mwendelezo ya mafanikio hayo. Hakika, mimi Daudi Gamba Machumu, mmiliki wa BP  nimetoa mchango mkubwa katika kizazi cha kipndi hiki.

Miongoni mwa nafanikio yangu ni pamoja na:

1: Jamii kutambua mchango wangu kwa kupata huduma ya chakula cha asili, yaani chenye kionjo na mkono wa utamaduni wa Kiafrika.

2: Kurudisha utamaduni wa kuvithamini na kuvienzi vitu vyetu vya asili zamani vilivyokuwa vikionekana vya kishenzi kwa jamii ya nje.

3: Kurudisha hadhi na utamaduni wetu kama Watanzania

4: Kukuza pato la mtu mmoja-mmoja na uchumi wa taifa kwa ujumla

5: Kuboresha mahusiano ya Watanzania katika ngazi mbalimbali kupitia biasharal.

6: Baishara kuzalisha ajira kwa jamii.

7: Kuikumbusha jamii kwamba chakula  kama mimea ni chanzo cha tiba ya magonjwa dhidi ya matumizi ya mafuta, vidonda vya tumbo, kisukari, n.k.

8: Tumekuwa liwazo la watu baada ya majukumu makubwa ya kazi kabla ya kwenda majumbani kwao kujipumzisha na kukabiliana na majukumu mengine.

9: Tumekuwa mfano wa kuigwa kwa watu wengine kuanzisha sehemu zao za biashara kama zetu.

Mfano wa watu walionufaika na maarifa kutoka kwetu ni pamoja na Dorka Catering na  Sofia Chef Sea Cliff Karambezi Restaurant.

10: Familia yangu imejitanua kielimu  kwa ajili ya biashara hii mbali na kwamba nimejuana na watu wengi kuanzia ngazi ya uraisi mpaka ngazi ya shina nchini  Tanzania  na  nje, wakiwemo mwanasiasa maarufu wa Kenya, Mheshimiwa Raila Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, Mheshimiwa William Ruto, na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, na Rais Mokgwesti Masisi wa Botswana.

Na Msimulizi Wetu

Leave A Reply