The House of Favourite Newspapers

Nilifanya Mapenzi na Maiti 20 Nitajirike – 7

maiti-cover

 ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA

Akaniambia twende sehemu kuzungumza, kwanza niliogopa lakini sikuwa na jinsi, ningefanya nini na wakati nilihitaji msaada mkubwa kutoka kwake? Hivyo nikakubaliana naye. Tukaenda sehemu, ilikuwa pembeni ya duka moja la vinywaji, pale niliona kukiwa na mikeka zaidi ya thelathini ikiwa imekunjwa, sikujua ilikuwa ni ya kazi gani.

“Unajua mpango mzima wa kulala humu?” aliniuliza swali.

“Kulala humu? Kwani kuna watu wanalala humu?” nilimuuliza huku nikionekana kushtuka.

MWAGIKA NAYO HAPA….

“Ndiyo! Wanakodisha mikeka na kulala, saa kumi na mbili wanairudisha..” aliniambia.

“Wanakodisha wapi?”
“Hapa kwangu…ukitaka nitakupa…”
“Wanakodisha kwa shilingi ngapi?”
“Elfu moja, ila wewe, nitakufanyia bure kabisa…” aliniambia.

Jibu lake lilinipa uhakika juu ya kile nilichohisi juu yake. Sikutaka kukataa, nilikuwa na uhitaji mkubwa wa kukaa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuutafuta utajiri hivyo nilikubaliana naye. Akanipa mkeka na kunionyeshea sehemu ya kulala, nikaenda, nikautandika na kulala huko.

Maisha yangu mapya yakaanza ndani ya kituo hicho, nilishinda nikiwa huko, sikutoka kwani mambo mengine nilikuwa nikiyafanya humohumo ndani. Mwanaume huyo aliyeitwa Dickson akanitafutia biashara ya kuuza ya kuuza magazeti, kweli nikaanza kuifanya na kuingiza kiasi kidogo cha fedha, hichohicho ndicho nilichokitumia kwa matumizi mengine.

Dickson alinionyeshea upendo wa ajabu, alionekana kuwa miongoni mwa wanaume waliokuwa na uvumilivu mkubwa. Hakuniambia suala lolote la kimapenzi, wakati mwingine nilikuwa nikijiuliza sababu ya yeye kunisaidia, kwa nini mimi? Je hali ingeendelea hivyohivyo au mwisho wa siku angebadilika.

Mwezi wa kwanza ukapita, nilikuwa nikiendelea kuishi ndani ya kituo hicho na kwa kweli sikuwa nimetokea. Ninayokuandikia hapa unaweza ukashangaa lakini ukweli ulikuwa huo. Ulipoingia mwezi wa pili, Dickson akashindwa kuvumilia, akaniambia ukweli kwamba alikuwa akinipenda na alitaka kunioa.

“Kunioa mimi?” niliuliza.

“Ndiyo!”

“Hapana! Haiwezekani…”

“Kwa nini?”

“Dickson, nipo tayari kwako kwa kila kitu isipokuwa mambo mawili tu,” nilimwambia pasipo kumuonea aibu.

“Mambo gani?”
“Sitaki unioe na sitaki uzae nami, ila mengine yote ruksa…” nilimwambia bila kupepesa macho.

Akatabasamu kidogo na kuniangalia kwa macho yaliyoonyesha kama mtu aliyetaka nirudie kauli zangu. Hakuniambia kitu zaidi ya kuondoka kuendelea na shughuli zake huku mimi nikiendelea kuuza magazeti.

Ilipofika usiku, akaniita alipokuwa akilala na kunitaka nimpe kampani kwani usiku huo ulikuwa na baridi kali hivyo nikakubaliana naye na kwa mara ya kwanza kukutana naye kimwili. Moyoni sikuumia, sikujuta kwani tangu nimeingia Dar es Salaam ndiye aliyeonekana kuwa msaada wangu mkubwa.

“Zakia…” aliniita kwa sauti ya uchovu.

“Abee mpenzi…”

“Nataka uwe tajiri kama unavyosema, upo tayari?” aliniuliza huku akiuweka mkono kifuani kwangu. Kabla ya kujibu, nikaachia tabasamu pana.

“Nipo tayari!”
“Kweli?”
“Ndiyo mpenzi! Nimesafiri kutoka Morogoro kuja hapa kwa ajili hiyo tu…” nilimwambia.

“Basi subiri..kesho kuna mtu atakuja, mwambie kila kitu,” aliniambia.

“Anao utajiri?”
“Hana ila ukitaka, anakupa?”
“Kweli?”
“Hakika!” aliniambia huku akiongeza tabasamu usoni mwake. Nikawa na uhakika wa kuuupata huo utajiri.

Nilikaa pale Ubungo na kuanza kumsubiria Dickson ambaye aliniambia asingechukua muda mrefu mpaka kurudi mahali hapo. Kama nilivyokwambia kwamba nilikuwa na presha kubwa, hakukuwa na kitu kingine nilichokifuata jijini Dar es Salaam zaidi ya utajiri tu, hivyo kuniambia kwamba angerudi akiwa na mtu ambaye angenifanya nitajirike, kwangu ilikuwa furaha tele.

Nilikuwa na presha kubwa, kila wakati nilikuwa nikiangalia saa yangu, hakukuwa na siku ambayo niliona mshale wa dakika ukienda taratibu kama siku hiyo, nilikuwa na presha kubwa na kitu nilichokitaka kwa wakati huo ni kuonana na huyo mtu na kumwambia kile nilichokitaka.

Baada ya kusubiri kwa saa tatu ndipo Dickson akarudi huku akiwa na huyo mtu. Alikuwa mwanaume mtu mzima, mwenye ndevu nyingi ambaye alionekana kuwa wa kawaida sana kiasi kwamba nikashangaa, iweje mtu huyo anipe mimi utajiri na wakati yeye mwenyewe alionekana kuwa mtu wa kawaida sana.

Wakati nikijiuliza hayo yote, mwanaume huyo, hata kabla ya kuzungumza nami, akatoa tabasamu pana usoni mwake, tabasamu lililoonyesha matumaini makubwa kwamba nisiwe na wasiwasi kwani tayari nilipata nilichokitaka.

“Naitwa bwana Hassani Mudi…” alijitambulisha huku akiniangalia kwa uso wenye tabasamu hilo pana.

“Naitwa Zakia…” nilimwambia, na mimi nikatoa tabasamu pana vilevile.

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia kesho hapa kujua kitakachoendelea katika sehemu ya NANE.

MWANDISHI: NYEMO CHILONGANI

halotel-strip-1

 

Comments are closed.