The House of Favourite Newspapers

Niliolewa na Mganga kwa Tamaa ya Cheo

0

ILIPOISHIA:

Nilisimamisha gari ili nipate uhakika na kauli ya babu kuwa anajua vitu vingi pia aliwahi kumiliki magari. Tulipishana babu alikaa kulia na mimi kushoto, mwanaume alikanyaga mafuta kama hana akili nzuri. Babu alikuwa fundi wa kuendesha gari kama kazaliwa nalo.SASA ENDELEA…

Tuliwahi kuingia mjini tofauti na mwendo wangu, nilimuuliza hoteli ambayo tutafikia kama anaijua. Sikuamini alinitajia mpaka ilipo, nilimweleza hapo ndipo tutalala. Alilipeleka gari mpaka kwenye hoteli hiyo tuliteremka kama bibi na bwana na kuelekea ndani.

Kutokana na jinsi alivyokuwa alionekana ni mzee mwenye fedha zake hasa kutokana na bakora aliyokuwa ameshika mkononi ilionesha ilikuwa ya gharama kubwa. Babu alinieleza bakora ile ilikuwa ya gharama kubwa alipewa zawadi na tajiri mmoja alipokwenda kufanya kazi ya uhakika Uarabuni. Kwa kweli siku hiyo babu alipendeza sana.

Nilikwenda mapokezi kuchukua funguo kisha tuliongozana na babu hadi katika chumba nilichokikodi kwa kazi maalum siku tatu. Tulikwenda hadi chumbani, babu hakuwa mgeni maeneo yale hakuonesha kushangaa kama wengi tukiingia kwa mara ya kwanza sehemu kama zile.

Nakiri tangu nivunje ungo sikuwahi kupata mapenzi yaliyousuuza moyo wangu kama siku ile. Nilijikuta nikipata wivu na kuona kina Rose wanafaidi penzi shatashata la babu kwa kulipata kwa wakati. Siku ya pili niliamka nikiwa nipo hoi bin taabani kutokana na uchovu wa mshikemshike wa usiku.

Lakini kwa vile nilitakiwa nifike ofisini kuchukua tiketi na viza kwa ajili ya safari, nilitoka na kuelekea ofisini. Kutokana na uchovu nilifika saa tano asubuhi.
Nilipofika mapokezi ya kuingia kwa mkurugenzi nilikutana na shoga yangu Safia aliyekuwa bize, aliponiona aliacha kazi na kunigeukia.

“Waaaooo shoga za nyumbani?”
“Nzuri, naona unawajibika.”

“Niende wapi sisi ni wa hapahapa chezea elimu wewe?”
“Hakuna dada pia elimu haina mwisho ni kujiongeza tu, vipi bosi yupo?”
“Yupo, mambo mazuri.”
“Mmh!”

Niliguna huku nikigonga mlango na kuruhusiwa kungia, mbele kwenye meza kuu alikuwa amekaa mkurugenzi aliponiona kwa mara ya kwanza alinyanyuka kunikaribisha.
“Karibu Eflazia.”
“Asante bosi.”

Tulizungumza mawili matatu mazungumzo ya kimaisha huku akinieleza posho ninayoipata nisijisahau kwa vile kuna maisha nje ya kazi. Nilimweleza hata mimi sikujisahau kwani wakati huo nyumba yangu nilikuwa namalizia ambayo ilikuwa ikisimamiwa na mama yangu.

Niliamini mpaka narudi masomoni nyumba yangu itakuwa imekwisha pia kodi yangu sehemu niliyopangishiwa ingekuwa imebakiza miezi sita kumalizika.

Baada ya mazungumzo alinipatia tiketi na paspoti yangu yenye viza tayari. Nilichukua vitu vyangu na kumuaga bosi na kunitakia maandalizi mema ya safari huku akiomba kama kuna tatizo nisisite kumjulisha ili kuhakikisha safari yangu nakwenda bila tatizo.

Mapokezi nilikutana na shoga yangu Safia aliyetaka kujua nini kimejiri ndani japokuwa alikuwa akijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
“Vipi shoga nina imani mambo yamekwenda vizuri.”
“Namshukuru Mungu yamekwenda vizuri.”

Kwa vile mwili ulikuwa umechoka kwa kazi ya usiku niliagana naye ili nirudi kupumzika. Nilipotoka pale nilirudi hotelini kulala, nilimkuta babu kajilaza kitandani akiangalia tivii akiwa amejifunga taulo kifua wazi.

“Karibu mjukuu,” babu alinikaribisha kwa bashasha tofauti na mwanaume wangu alikuwa mwingi wa heshima kama mtu na mwanaye lakini kwa babu haikuwa hivyo. Alikuwa amechangamka na kunifanya nijiulize ujana wake alikuwaje.

Kwa kweli siku mbili nilizokuwa na babu nilifaidi sana na kutamani kila siku niwe naye, lakini kwa vile nilikuwa na safari muhimu sikuwa na budi kuachana naye na kupanga nikirudi tuliendeleze penzi letu. Kwa vile ilikuwa imebakia siku moja ya maandalizi ili siku inayofuata niondoke nilimrudisha babu kijijini.

Siku ile nilimpekeka jioni kutokana na mchana kuwa na kazi moja ya burudani ya bandika bandua. Baada ya kumfikisha babu sikukaa niligeuza kwani mwili haukuwa wangu nilihitaji kupumzika kwa siku moja kabla ya siku inayofuata majira ya saa mbili usiku niondoke kwenda masomoni.

Nilipofika nyumbani niliwaeleza wadogo zangu ambao ndiyo ningewaacha kulinda nyumba kipindi chote nitakachokuwa masomoni. Niliwaeleza wasiniamshe mpaka nitakapoamka mwenyewe.

Niliingia ndani na kujitupa kitandani, licha ya kuwa burudani lakini iliniacha hoi. Niliamka saa sita usiku nikiwa na njaa kali. Nilipata chakula kisha nilioga na kurudi kitandani, kutokana na uchovu nilipogusa kitanda usingizi mzito ulinichukua.

Huwezi kuamini usiku mzima njozi zote zilikuwa kwa babu Sionjwi mpaka kunakucha.

Je, kilifuatia nini? Usikose kupata mwendelezo wake katika Gazeti la Risasi Jumamosi.

Leave A Reply