The House of Favourite Newspapers

Ninja Arejea Mdogomdogo Yanga

 

BAADA ya kuikosa michuano ya Kombe la Mapinduzi, beki wa kati wa Yanga, Abdallah Saibu ‘Ninja’, amepata nafuu ya majeraha ya kifundo cha mguu na wiki hii anatarajiwa kuanza programu maalumu ya Mazoezi mepesi ya binafsi.

Beki huyo, Alipata majeraha hayo kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kumalizika kwa Yanga kufungwa mabao 2-0.

Akizungumza na Championi Jumatatu, meneja wa timu hiyo, Hafi dh Saleh, alisema beki huyo akiwa nje ya uwanja anaendelea kufanya mazoezi kwa programu maalumu aliyopewa na daktari, Edward Bavu katika kuhakikisha anapona kwa haraka.

Saleh alisema beki huyo ataendelea kufanya program hiyo kwa muda wa wiki moja kabla ya kurejea uwanjani kuanza mazoezi ya nguvu pamoja na wenzake.

 

Aliongeza kuwa, kuumia kwa beki huyo kumeharibu mipango ya kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa aliyepanga kumtumia Ninja katika Kombe la Mapinduzi kwa ajili ya kumuongezea uzoefu na hali ya kujiamini kama walivyokuwa wachezaji wengine ambao hawakutumika sana katika ligi kuu.

 

“Ninja hakutumika katika ligi kuu kama benchi la ufundi lilivyopanga kuwatumia wachezaji ambao hawakupata nafasi katika mechi za ligi kuu kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.

“Hivyo, ni jambo jema hivi sasa ameanza kupata nafuu na kuanza mazoezi mepesi ya binafsi akifuata program maalumu aliyopewa na daktari wa timu, Bavu.

 

“Tuna matarajio makubwa ya kuwa fi ti zaidi na kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake wiki ijayo akiwa amepona kabisa,” alisema Saleh.

 

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.