The House of Favourite Newspapers

Nisha Amempiga Dongo Wolper Kuhusu Serengeti Boy?

0
Alichokiandika Nisha.

 

STAA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu almaarufu Nisha Bebe staa, amesema hawezi kutoka na vijana wenye umri mdogo kumzidi (Serengeti Boy) kwa kile alichosema Serengeti ameiachia mbuga.

Walichokijibu mashabiki.

 

Nisha ambaye yupo kimya kidogo katika muvi kwa vile yuko bize na biashara zake za nguo, alitoa kauli hiyo kupitia mtandao wake wa Instagram bila kumtaja mtu, lakini baadhi ya mashabiki wakatoa maoni yao na kusema hilo ni dongo kwa msanii mwenzake wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper ambaye kwa sasa anakula maisha na ‘dogo’ anayejulikana kwa jina la Brown ambaye pia ni mwanamitindo.

 

Wolper na mpenzi wake wa sasa Brown.

 

Bado haijafahamika na Nisha hajawa wazi kwamba dongo lae amemlenga nani kutupia maneno hayo aliyoyatoa.

NA ISRI MOHAMMED | GLOBAL PUBLISHERS

Usipitwe, Pata Notifications za Matukio Yote Kutoka GLOBAL TV ONLINE

Leave A Reply