The House of Favourite Newspapers

Niva Ampigia Saluti Gabo

0

Na Mwandishi Wetu

ZUBERY Mohamed ‘Niva’ ambaye ni mmoja wa waigizaji wa kitambo Bongo, amempigia saluti muigizaji bora wa kiume kwa sasa nchini, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ kwamba hana mpinzani kutokana na uwezo mkubwa alionao.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Niva alisema anafahamu uwezo alionao, lakini kushiriki kazi moja na Gabo ni lazima msanii akaze msuli kwa sababu ana ujuzi mkubwa na ni mwenye kubadilika badilika kwa kila filamu anayocheza, kitu kinachomfanya akose mpinzani kwa sasa.

“Ingawa nimeuona uwezo wake muda mrefu, lakini baada ya kushiriki naye filamu ya Kasanga Naye Mwana, ndipo nimegundua kuwa jamaa kwa sasa hana mpinzani, licha ya kwamba humo ndani nimefanya vitu vikubwa, watu kama hawa wanatakiwa kwenye tasnia ili kuirejesha kileleni,” alisema Niva, ambaye filamu yao hiyo itaingia mtaani baadaye mwezi huu.

Leave A Reply