The House of Favourite Newspapers

Niyonzima apangiwa mlo maalum amzuie Tchetche

0

NIYONZIMA (3) Wachezaji wa Timu ya Yanga wakifanya Mazoezi.

Wilbert Molandi,
Dar es Salaam
YANGA haitaki mchezo kwani imempangia mlo maalum kiungo wake Haruna Niyonzima ili aweze kupambana ipasavyo na wachezaji wa timu pinzani katika Ligi Kuu Bara, akiwemo Kipre Tchetche wa Azam FC.

NIYONZIMA (7)

Haruna Niyonzima.

Ili mambo yaende vizuri, Daktari wa Yanga, Nassoro Matuzya, amempangia mlo kamili wa vitamin Niyonzima kwa lengo la kujenga mwili wake uwe tayari kwa mapambano muda wote.
Yote hayo yamefanyika siku chache baada ya Niyonzima kurejeshwa kikosini na uongozi kutokana na kusimamishwa kwa kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Niyonzima, raia wa Rwanda, alikaa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja huku wenzake wakiendelea na programu za mazoezi chini ya kocha Hans van Der Pluijm.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema: “Nilizungumza na daktari baada ya kuona stamina, pumzi na matumizi ya nguvu kwangu yapo chini, sasa nimepangiwa mlo maalum ili kujenga mwili.
“Nimepangiwa chakula maalum ambacho kitanisaidia kurejea katika hali yangu ya siku zote na hapo nitakuwa fiti kupambana na wachezaji wa timu pinzani katika mechi zetu.
“Natakiwa kula vyakula vyenye vitamin kwa ajili ya kurudisha mwili wangu, fiziki, stamina na pumzi baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.”
Tayari Niyonzima ameichezea Yanga mechi moja baada ya kurudishwa kundini ambayo ni Kombe la FA dhidi ya Friends Rangers ambapo Wanajangwani walishinda mabao 3-0 Jumapili iliyopita.

Leave A Reply