The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Chama Anajua Ila Namzidi Hapa…

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima amekiri kwamba kiungo mwenzake, Claytous Chama anaujua mpira vizuri lakini anamzidi uwanjani kwa sababu yeye ni mwepesi kuliko Mzambia huyo.

Chama tangu ametua Simba akitokea Power Dynamos ya kwao Zambia amekuwa akifananishwa kiuchezaji na Niyonzima ambaye msimu huu mambo ‘yamemkalia kushoto’ baada ya kukosa nafasi ya kucheza sana.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Niyonzima amesema yeye na Chama ni marafiki wakubwa na wamekuwa wakizungumza vizuri tofauti na wengi wanavyodhani yeye yuko juu zaidi ya Mzambia huyo kwa sababu mambo anayoyafanya uwanjani anafanya kwa utaratibu tofauti na yeye ambaye yuko fasta.

“Chama ni kiungo mzuri sana na anaujua mpira na mara nyingi tumekuwa tukizungumza vizuri kuhusiana na masuala ya uwanjani tofauti na watu wanavyoona kwamba eti sisi ni maadui.

 

“Hatufanani kiuchezaji kwa sababu yeye vile vitu anavyofanya uwanjani anafanya kwa uzito fulani hivi tofauti kabisa na mimi ambaye ninafanya hivyohivyo lakini kwa uharaka zaidi, hivyo hatuwezi kuwa sawa hata kidogo,” alisema Niyonzima.

Said Ally na Musa Mateja, Dar

Comments are closed.