The House of Favourite Newspapers

JPM AKAGUA MAGARI YA JESHI YATAKAYOSOMBA KOROSHO “SITIKISIKI HATA IWEJE” – VIDEO

Rais John Magufuli leo Jumamosi, Novemba 10, 2018 amekagua magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ ambayo yanaweza kutumika kubebea korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara iwapo wanunuzi binafsi wa zao hilo hawatatii maagizo ya Serikali ifikapo Jumatatu, Novemba 12, 2018 saa 10:00 Jioni, kama alivyoagiza jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mhe.Rais Magufuli amefanya ukaguzi huo katika Kambi ya Jeshi ya Twalipo, Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Mgulani Jijini Dar es Salaam ambapo magari 75 yenye uwezo wa kubeba tani 1,500 kwa mpigo yameandaliwa kwa ajili ya kubeba korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na Tanga.

Majaliwa alitoa siku nne kuanzia jana Ijumaa hadi Jumatatu ijayo, Novemba 12, kwa wanunuzi wote wa korosho kupeleka barua ofisini kwake kuonyesha tani wanazohitaji na lini watazichukua.

Alisisitiza kwamba  baada ya hapo hawatanunua tena korosho hizo na watafutiwa usajili wa ununuzi wa zao hilo.  Hali hii imetokana na sintofahamu kwenye minada ya zao hilo kuu la biashara  nchini.

“Mimi ni askari niliyeiva huwa sitikisiki hata kwa upepo wa aina gani” amesema Dkt. John Pombe Magufuli, Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

VIDEO: TAZAMA MAJALIWA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.