The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Tutapoza Machungu Na Mapinduzi

NIYONZIMA (7)

 Kiungo wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

Said Ally na Omary Mdose; Championi Jumatano
KIUNGO wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, ameweka bayana kwamba hawatarudia uzembe walioufanya katika msimu uliopita katika Kombe la Mapinduzi jambo ambalo liliwagharimu na kujikuta wakilikosa taji hilo.

Yanga inatarajiwa kushiriki Kombe la Mapinduzi ambalo litaanza kuunguruma Desemba 30, mwaka huu huku kikosi hicho kinachonolewa na Mzambia, George Lwandamina kikiwa kimepangwa Kundi B, sambamba na timu za Azam, Zimamoto na Jamhuri.
Niyonzima ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, ameliambia Championi Jumatano kuwa kwa sasa hawataangalia aina gani ya kombe ambalo wanalipigania, bali watajituma na kuhakikisha wanalitwaa.

NIYONZIMA (5)
“Hatuwezi kulidharau Kombe la Mapinduzi kama ilivyokuwa msimu uliopita jambo ambalo lilifanya tutolewe na kulikosa, msimu huu hatutaki masihara hata kidogo na tutaanza na kombe hilo kisha mengine yatafuata.
“Tumepanga tutwae kila ubingwa katika michuano tutakayoshiriki msimu huu na hilo linawezekana kwa sababu tuna kikosi imara na kocha mwenye uwezo wa hali ya juu,” alisema Niyonzima ambaye kwa sasa ndiye nahodha wa Yanga.

Comments are closed.