The House of Favourite Newspapers

Njemba Ala Kichapo ‘Hevi’ Standi Ya Daladala Mchana Kweupe

njemba-2Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiendelea kupewa kichapo hevi mchana kweupe baada ya kudaiwa kuiba Headphone za simu zenye thamani ya shilingi 2000 mjini Morogoro.

njemba-3 njemba-4 njemba-5 njemba-6Wananchi wenye hasira kali wakiendelea kumpa kijana huyo kijachapo.

njemba-7

Wananchi wenye huruma wakimsadia kijana huyo baada ya kula kichapo.

njemba-1Baada ya kumuokoa kijana huyo baada ya kichapo.

MOROGORO: Katika hali ya kushangaza kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, amenusurika kifo baada ya kupokea kichapo kizito kutoka kwa kundi kubwa la wananchi wenye hasira waliomtuhumu kuiba Headphone za simu zenye thamani ya shilingi 2000.

Tukio hilo lililoshuhudiwa ‘live’ na Risasi Jumamosi lilitokea Jumatatu ya wiki hii majira ya mchana katika stendi ya daladala iliyopo katikati ya Mji wa Morogoro.

Wakizungumza na mwandishi wetu, mashuhuda wa tukio hilo Maga Juma na Twaha Omar ambao ni madereva wa daladala walisema:

“Kama unavyoona hapa stendi Wamachinga ni wengi wakifanya biashara zao, huyu jamaa alitaka kununua Headphone za simu za buku 2 akawa anazuga kuigeuzageuza baadaye wakaja wateja wengine wakichagua vifaa vingine kwa huyo chinga jamaa alivyoona chinga yuko bize na wateja wengine akatumia mwanya huo kuzificha mfukoni na kuondoka zake,” alisema Twaha na kuongeza:

“Chinga alikuwa makini na biashara yake akamshtukia alivyomwita huyu jamaa akakimbia na kama unavyojua stendi watu wengi, wananchi wamemkamata na kumshushia kichapo aliposachiwa amekutwa na hiyo Headphone ameificha kwenye mfuko wa pensi aliyovaa,” alisema Twaha.

Naye Maga Juma alisema:

”Huyu jamaa kama siyo huyu askari kanzu aliyefika eneo la tukio na kumuokoa angeuawa kwani wakati wananchi wanampiga naye anarusha ngumi kujibu mapigo kwenye kundi hilo la wananchi ambao kwa hasira waliamua kuchukua silaha mbalimbali yakiwemo mawe na kumtwanga mwilini,” alisema Maga. 

Mwandishi wetu alishuhudia jamaa mmoja aliyevalia kiraia aliyejitambulisha kwamba ni askari ambaye alifanikiwa kumchomoa jamaa huyo kwenye kundi la wananchi na kuelekea naye kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

(PICHA/ HABARI: DUSTAN SHEKIDELE, RISASI JUMAMOSI/GPL)

Comments are closed.