The House of Favourite Newspapers

Yanga, Azam Hakuna Mbabe Watoka Suluhu

yanga-1Kikosi cha timu ya Yanga kilichoanza dhidi ya Azam leo Uwanja wa Uhuru.

yanga-2

Kikosi cha timu ya Azam kilichoanza leo dhidi ya Yanga.

yanga-3

Beki wa Azam, Aggrey Moris (kulia) akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa.

yanga-4

Wachezaji wa Yanga wakijiaandaa kuunganisha mpira wa kona huku wale wa Azam wakiwazuia

yanga-5

Purukushani uwanjani

yanga-6

Mlinzi wa Yanga, Hajji Mwinyi (jezi no 20) akiufuata mpira

yanga-7

Chirwa akijaribu kumtoa beki wa Azam, Danniel Amoah

yanga-8

Mchezaji wa Azam akiwaamua Juma Abdul na Amoah 

yanga-9

Wachezaji wa Yanga wakimzonga mchezaji wa Azam

yanga-10

Mashabiki wa Yanga wakishangaa baada ya Msuva kukosa bao (hayupo pichani).

yanga-11

Viungo Thaban Kamusoko akipambana na Sure Boy wa Azam

yanga-12

….wakiwania mpira

AZAM ikiwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Uhuru mbele ya Yanga imeshindwa kubakiza alama tatu baada ya mchezo wao kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo huo ambao ulijaa ubabe mwingi, ulishuhudia mwamuzi Israel Nkongo akitoa kadi za njano tano huku nne zikienda kwa Azam na moja kwa Yanga.

Katika mchezo huo washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Donald Ngoma wa Yanga na wale wa Azam waliokuwa chini ya nahodha John Bocco walikosa nafasi nyingi za kufunga mabao lakini uwezo wa makipa wa timu zote uliwafanya washindwe kutikisa nyavu zao.

Takwimu zinaonyesha Azam walicheza faulo 17 na Yanga 10, mashuti yaliyopigwa na Azam na kulenga lango yalikuwa matano kwa Azam na Yanga sita.

(PICHA: RICHARD BUKOS/GPL)

Comments are closed.