The House of Favourite Newspapers

Njemba Azama Baada ya Lami Kuyeyuka Barabarani

KIJANA mmoja mwenye umri wa miaka 24, nchini Uingereza amewashangaza wengi baada ya kuzama kwenye lami iliyokuwa imeyeyuka barabarani eneo la Heaton jijini Newcastle wakati akielekea dukani.

 

Imeelezwa kwamba, Mguu wake ulikuwa umetumbukia hadi karibu paja katika ndipo aliwapigia maofisa wa huduma za dharura kupitia nambari 999 ambao baada ya kufika walilazimika kuchimbua barabara eneo alipokuwa amekwama wakitumia nyundo na patasi kuutoa mguu wake.

Maofisa hao wanasema aliokolewa bila jeraha kutokana na hali kwamba alikuwa amevalia “buti la babu yake aina ya Dr Martens” ambazo hufika hadi magotini huku wakidai kwamba tukio hilo lilisababishwa na jua kali ambalo limekuwa likiwaka eneo hilo.

 

Kisa hicho kimetokea siku chache baada ya lori la kusafirisha taka kudidimia kwenye barabara moja ya lami Newbury, Berkshire ambapo maeneo mengi Kaskazini na Kusini mwa Dunia yamekuwa yakishuhudia jua kali.

Nchini Australia, wenye magari katika eneo la Atherton Tablelands jimbo la Queensland walilazimika kuyaacha magari yao baada ya lami kuanza kuyeyuka barabarani. Tairi za magari ziliharibiwa vibaya na lami na sasa madereva takriban 50 wanadai fidia.

 

Maofisa wanasema kisa hicho kilisababishwa na jua kali, pamoja na hali kwamba ukarabati ulikuwa umefanyika wiki iliyopita. Nchini Canada, watu 33 wamefariki dunia wiki hii baada ya kutokea kwa joto kali katika maeneo ya kusini mwa Quebec.

Joto kali lilianza Ijumaa ambapo kiwango cha joto kilifikia 35C (95F) pamoja na kiwango cha unyevu kwenye hewa kupanda. wengi wa waliofariki ni wa kati ya miaka 50 na 80. Wakazi wamehimizwa kunywa maji kwa wingi na kukaa kivulini. Watu 18 kati ya hao waliofariki walikuwa jijini Montreal.

Kiwango cha joto mjini humo wakati kama wa sasa huwa ni 25C. Lami kwenye barabara nyingi huweza kuyeyuka kiwango cha joto kikifikia 50C. Takriban 5% ya barabara 80C. Barabara za lami hushika joto sana na hivyo kiwango chake cha joto kinaweza kufikia 50C jua kali likiwaka.

Comments are closed.