The House of Favourite Newspapers

Njia za Kutoka Jela Shamim Mwasha na Mumewe

0

NJIA za kumuwezesha Shamim Mwasha na mumewe Abdul Nsembo waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani Machi 31, mwaka huu ni mbili.Ya kwanza, ni kushinda Rufaa endapo wataamua kufanya hivyo, ikishindika huruma ya rais kuwatoa gerezani itakuwa ndiyo karata yao ya mwisho.

 

Tofauti na hapo maisha yao yatakuwa gerezani hadi watakapomrudia Mungu.Kulala na kuamkia gerezani hadi kifo, huwenda hiki ndicho kinachowaliza ndugu na jamaa zao.

 

Ingawa baada ya hukumu kutoka Nsembo alijipiga kifua na kuwatuliza waliokuwa wanawalilia kwa kuwaambia hukumu ya Jaji mmoja (Elinaza Luvanda) isiwatishe, akimaanisha watakata rufaa.

 

Hata hivyo, mambo yote mawili hayaonekani kuwa mepesi, kwani kushinda rufaa siyo jambo rahisi na hata kusamehewa na rais kwa kosa hilo siyo kitu cha kukitumaini sana.

 

Mtazamo huu ndiyo uliowasukuma wengi kuwaonea huruma licha ya kosa walilokutwa nalo la kujihusisha na biashara ya madaya ya kulevya aina ya heroin.

 

Machozi na masikitiko mengi yameelekezwa kwa watoto wa watuhumiwa hao ambao wamebaki uraiani kama yatima.“Hivi kweli Shamim alikuwa anauza madawa ya kulevya? Nakataa.” Mchangia mmoja kwenye mtandao wa kijamii aliandika, akichagiza mjadala lioshika kasi kwenye ulimwengu wa mitandao kwamba huwenda mwanamke huyo alinaswa na mtego ambao hakuujua.

 

Lakini pamoja na yote wakili wa Shamim, Hajra Mungula alishindwa kuijengea hoja Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi), ili kumnasua na kinachosemwa.Lakuamini limebaki kuwa hilo la uamuzi wa mahakama, mengine ya kushinda rufaa yanaweza kufuata.

 

Toleo lililopita la Jarida hili lilikuwa na makala ya kuwaonya wanawake kujichunga na wanaume wanaoonekana wana fedha kwani kuna kundi la wanaume limeibuka na kuwatumia wanawake katika biashara za madawa ya kulevya.

 

Pengine onyo hili libaki kuwa hai miongoni mwa wanawake wa Bongo, tofauti na hapo wataendelea kuliliana kila siku machozi hasiyoisha.Ikumbukwe kuwa Shamim alikuwa mjariamali na mmiliki wa blog maarufu ya masuala ya urembo ya 8020, sasa kama hakutosheka na yote, basi majuto kwake yatakuwa ni mjukuu.

Leave A Reply