The House of Favourite Newspapers

NMB Yaahidi Makubwa Kikao Kazi Cha Maofisa Wa Polisi

Kutoka kulia ni Kamishna wa Police, Operesheni na Mafunzo, Liberatus Sabas, Kamishna Msaidizi Mwandamizi: Mipango na Bajeti- Yustus Kamugisha, Kamishna wa Polisi  Inteligensia, Charles Mkumbo, Kamishna Msaidizi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana katika picha ya pamoja na Mkuu  wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo baada ya kikao kazi cha Maofisa wa Polisi kilichofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay,Dar es Salaam
Maafisa wa Benki ya NMB Ally Ngingite(Kushoto) na Isaac Mgwassa wakibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji, Semiyono.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamdan akifurahia jambo na Afisa wa benki ya NMB Amanda Feruzi.

 

BENKI ya NMB, imewahakikishia askari wa Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa Serikali nchini, huduma bora, rafiki na
sahihi za kibenki, zitakazokuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, ili kuendana na kasi ya maendeleo
kuelekea Uchumi wa Kati.

 

Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi na Kati wa NMB, Ally Ngingite, katika siku ya pili
ya Kikao Kazi cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa na Vikosi,
kinachofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

 

Kikao Kazi hicho kiliozinduliwa Septemba 24 na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, kimefika ukomo jana Ijumaa Septemba 27, 2019 ambapo kwa siku nne maofisa hao wamejadili juu ya mafanikio, changamoto na
mikakati ya Kamisheni katika Kuzuia, Kupambana na Kutanzua Uhalifu.

 

Kupitia Kikao Kazi hicho kinachofanyika chini ya Kaulimbiu: Umoja Wetu Ndiyo Nguvu Yetu, Tudumishe Usalama
Katika Uchumi wa Viwanda, wadau wa Jeshi la Polisi wamealikwa kushiriki, ikiwemo NMB iliyotoa ahadi ya
ushirikiano wa kudumu, sambamba na huduma bora kwa askari polisi nchini.

 

Ngingite aliwataka maofisa na makamanda hao kuwa mabalozi wema wa benki hiyo kwa askari walio chini yao kote
nchini na kwamba wanapaswa kuifanya NMB kama mshirika wa kweli katika kujikweza kiuchumi kupitia mikopo na
aina nyingine za uwezeshaji kutoka katika benki hiyo.

 

“Makamanda na maofisa wote mlioshiriki Kikao Kazi hiki, mkitoka hapa huku mnafikiria namna sahihi ya kuboresha maisha yenu ya sasa na baadaye, kukuza pato lenu kuelekea Uchumi wa Kati, maana yake ni kuwa askari wote nchini walioko chini yenu watafikia kufanya hivyo pia.

 

“Unafuu wa huduma zetu kwa Askari wa Jeshi la Polisi, majeshi mengine na Wafanyakazi wa Serikali, unatokana na
ukweli kwamba tunatambua, kuthamini na kujali mchango wenu kwetu kama taasisi ya kifedha,” alisema Ngingite,
ambaye alipokea maoni mbalimbali kutoka kwa makamanda hao.

 

Aliwaomba askari hao wanapoamua kukopa, kuhakikisha wanaitumia mikopo hiyo kwa usahihi, na kwamba siri ya
mafanikio iko katika kufikiria kabla ya kukopa, kufanya uwekezaji mdogo baada ya kukopa ili kutanua pato lao na
hatimaye kupunguza makali ya marejesho.

 

Akizindua Kikao Kazi hicho juzi, IGP Sirro aliwataka askari hao kuhakikisha wanajitoa kadri wawezavyo katika
kulitumikia taifa na kwamba yeye anatamani kumaliza nafasi yake Jeshi likiwa na heshima, ambayo itapatikana kwa
kila mmoja kuacha unafiki, kwani likichafuka, watachafuka wote.

Comments are closed.