The House of Favourite Newspapers

NMB Yamwaga Madawati 730 Kwa Shule Za Msingi, Kiomboi

0

MNEJA WA NMB KANDA YA KATI AKIMKABIDHI MKURUNGENZI IRAMBA MADAWATIMeneja wa NMB Kanda ya Kati (kulia) akikabidhi madawati kwa Mkurugenzi Wilaya ya Iramba.WANAFUNZI SHULE YA KIOMBOI BOMANI WAKIWA WAMEKALIA MADAWATIWanafunzi wa Kiomboi Bomani wakiwa wamekalia madawati.WANAFUNZI WAKIPOKEA MADAWATI. 2jpgWanafunzi wakipokea madawati.

NMB imekabidhi madawati 730 yenye thamani ya shilingi milioni 75 kwaajili ya shule za msingi 15 zilizopo wilayani Kiomboi – Singida huku kila shule ikipata madawati 50.

Msaada huo ni moja ya ushiriki wa benki katika maendeleo ya jamii na hivyo kuhakikisha kuwa jamii inayoizunguka benki hiyo inafaidika kutokana na faida wanayoipata. Katika mpango wake, NMB imetenga asilimia moja ya faida inayoipata baada ya kodi ambayo ni zaidi ya  shilingi bilioni 1 kwaajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu.

Shule zilizofaidika na msaada huo ni : Wala, Kisonga, Kigulu, Ujungu, Luzilukulu, Kiomboi, Lulumba, Isui, Tulya, Kitukuta, Mugela, Msai, Masagi, Kinkungu na Mtekente.

nmbMANENO YA UTANGULIZI KUTOKA KWA MENEJA WA NMB KANDA YA KATI KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI 15 ZA WILAYANI KIOMBOI – SINGIDA – JANUARY 29   2016

 

Afisa Elimu wa Wilaya  ya Kiomboi – Clement Berege

Viongozi wa Serikali mlioko hapa

Walimu Wakuu wa Shule zote 15 mliopo hapa  

Wenyeviti wa kamati za Shule zote,

Meneja wa Tawi la NMB Kiomboi,

Wafanyakazi wa NMB,

Wageni waalikwa, mabibi na mabwana, itifaki imezingatiwa,

Habarini za Asubuhi.

Ndugu Mgeni Rasmi, kwa niaba ya uongozi wa Benki ya NMB, napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa kwa kutambua kuwa NMB ni benki iliyo karibu na wananchi na hivyo kuwa sehemu ya kwanza kuikimbilia ili kutatua changamoto za elimu hapa shuleni.

Changamoto za sekta ya elimu Tanzania kwa NMB ni jambo la kipaumbele, hii ni kutokana na ukweli kwamba elimu ni uti wa mgongo wa taifa lolote lile hapa duniani.

Sisi kama NMB tulipopata maombi yenu, tulifarijika na kuamua mara moja kuja kushirikiana na ninyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya elimu kwa watoto wetu hapa Kiomboi.

Tunakushukuru pia kwa kutambua kuwa NMB ni mahala sahihi pa kukimbilia, hiyo inaonesha kuthamini kwenu mchango wetu kama benki katika kuchangia maendeleo.

Leo tunakabidhi madawati 730 ambayo yatagawiwa kwa shule 15 za hapa kiomboi, hizi ni shule za msingi – Wala, Kisonga, Kigulu, Ujungu, Luzilukulu, Kiomboi, Lulumba, Isui, Tulya, Kitukuta, Mugela, Msai, Masagi, Kinkungu na Mtekente.

Madawati haya tunayokabidhi leo  ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata.

Kwa maana hiyo, NMB tumeamua kushirikiana na shule hizi za Msingi hapa Kiomboi na jamii yote inayozunguka shule hizi kwa kuchangia madawati ambayo tunaamini yatasaidia kuamsha ari ya wanafunzi kusoma na hivyo kuchochea ufauru wa wanafunzi kwani tunaamini sasa watasoma wakiwa katika mazingira bora kabisa.

Ndugu Mgeni Rasmi, NMB katika mipango yake imekuwa ikishiriki shughuli mbali mbali za kijamii, kama kusaidia sekta ya elimu, afya na pia kufariji jamii katika vipindi vya majanga mbalimbali kama mafuriko na ajali mbalimbali zinazogusa maisha ya watu wengi.

Kwa miaka kadhaa sasa, NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita Zaidi kwenye miradi ya elimu (Madawati na viti), afya (Vitanda na magodoro pamoja na mashuka) na kusaidia majanga yanayoipata nchi yetu. Tunatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni wetu.

Ingawa NMB inapokea maombi mengi sana kuchangia miradi ya jamii, benki imejikita Zaidi katika maeneo ya elimu, afya na misaada ya hali na mali katika nyakati ngumu kama za majanga.

Ndugu Mgeni Rasmi , kwa mwaka 2016, NMB imetenga Zaidi ya shilingi bilioni 1 kwaajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu. Kiasi hiki kinatufanya kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo ya jamii kuliko benki yoyote nchini.

Kwa taarifa tu, NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 170, ATM Zaidi ya 600 nchi nzima pamoja na idadi ya wateja inayofikia zaidi ya milioni mbili hazina ambayo hakuna benki hapa nchini yenye hazina kama hiyo.

Kwa kumalizia, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa shule hizi , wenyeviti wa kamati za shule kwa kuwa mstari wa mbele kuona kuwa shule hizi zinapata mafanikio ya hali ya juu kielimu na hivyo kuwa mfano bora hapa Tanzania.

Nashukuru sana kwa kunisikiliza na sasa nipo tayari kukabidhi madawati kwa mgeni rasmi kwa niaba ya shule hizi zote 15.

Wakati huo huo Nmb imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi million 25 kwa mkuu wa mkoa wa singida.Vifaa tiba hivi vimetolewa kwaajili ya hospitali ya mkoa wa Singida ili kupunguza uhaba wa vifaa tiba ambao umekua ukiikumba Hospitali hii. Vitanda, magodoro na mashuka  ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyo tolewa na NMB.

Akizungumza wakati wa makabidhiano Meneja wa Kanda ya Kati NMB  Bw.Stratoni Chilongola alisema “NMB inathamini wateja wake na ndio maana NMB imetenga Zaidi ya shilingi bilioni 1 kwaajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu. Kiasi hiki kinatufanya kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo ya jamii kuliko benki yoyote hapa nchini.”

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya hospitali ya mkoa Singida iliwagusa wananchi wengi ambao wameshukuru uwepo wa tawi  NMB Mkoani Singida.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Singida Mkuu wa Mkoa wa singida Bw. DR Parseko Vinsent Kone alishukuru uongozi wa Benki ya NMB kwa kuthamini wananchi wake na hivyo kujitolea vifaa vyenye thamani ya shilling Milioni 25. “wananchi wa Singida tunatakiwa kujivunia uwepo wa Benki hii katika mkoa wetu, Ni jambo la kipekee sana kupokea msaada mkubwa kama huu kutoka kwa wadau wa maendeleleo ndani ya jamii yetu. Naomba niwashukuru uongozi wa NMB lakini zaidi ya yote nawaomba wananchi tuvitunze vifaa hivi ili vitufae kwa muda mrefu.”

Leave A Reply