BENKI ya NMB imetoa msaada wa madawati 100 kwa shule za msingi mbili, vifaa vya ujenzi na vifaa vya hospitali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 25 katika Mikoa ya Pwani, Dodoma na Dar es Salaam.
Benki hiyo imetoa Madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa shule za msingi Masaki ya wilayani Kisarawe Mkoani Pwani na Shule ya Msingi Msimbazi Mseto za jijini Dar es Salaam.
Msaada Mwingine uliotolewa ni Mashuka kwaajili ya Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili –Moi ya Jijini Dar es Dalaam yenye thamani ya shilingi Milioni Tano, Magodoro na vitanda vya wajawazito kwa hospitali ya wilaya ya Kongwa vyenye thamani ya shilingi Milioni tano na vifaa vya ujenzi kwaajili ya shule ya msingi Songambele yenye thamani ya shilingi Milioni tano hivyo kufanya msaada wote kuwa wa shilingi Milioni 25.
Hata hivyo, huu ni mwendelezo wa benki kujali wateja na jamii inayozunguka matawi yake huku ikiamini kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wake wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni waliojiwekea.
Kwa mwaka huu 2018, Benki ya NMB imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kusaidia jamii katika Nyanja za elimu na afya pamoja na kusaidia vipaumbele vilivyowekwa na serikali kwenye elimu ikiwa ni pamoja na Tehama na maabara kwa shule za msingi na sekondari.
Comments are closed.