The House of Favourite Newspapers

NMB Yawakutanisha Wafanyabiashara Mkoani Tabora

0
Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magese akizungumza na wafanyabishara wa Mkoa
wa Tabora.

BENKI ya NMB inaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuhakikisha wanazielewa bidhaa na
mipango ya benki hiyo ili wanufaike na biashara zao.

Akizungumza katika warsha ya klabu ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Tabora, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya
Magharibi, Sospeter Magese,alisema kikao na wafanyabiashara ni muhimu katika kubadilishana mawazo.

Mwenyekiti wa Klabu ya wafanyabishara Mkoa wa Tabora, Michael Mambo akifungua warsha hiyo
iliyofanyika Mkoani Tabora.

 

Magese alisema warsha hio ambayo haijafanyika tangu mwaka 2019 kutokana na ugonjwa wa UVIKO19, imekuwa
na mafanikio makubwa kwa pande zote mbili na kuongeza kuwa wamepata fursa ya kuwaeleza wafanyabiashara
bidhaa zao ikiwemo riba ya asilimia tisa katika kilimo.

Alieleza kuwa Benki ya NMB imechukua changamoto zote zilizotolewa na wafanyabiashara hao na kuahidi kuwa
benki hiyo itazifanyia kazi haraka.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya wafanyabiashara hao,Michael Mambo,aliwataka wafanyabiashara kuacha uoga wa
kukopa kutoka taasisi za fedha huku akisisitiza kuwa mikopo ina manufaa makubwa na iheshimiwe huku akiwasihi
kutoitumia kinyume na malengo waliyokusudia.

Wafanyabishara katika warsha ya klabu ya wafanyabishara Mkoani Tabora iliyoandaliwa na benki ya NMB

Mfanyabiashara Elizabeth Nkonyoka alisema wamefurahi na kunufaika na warsha hiyo kwa kupata elimu ya
kifedha na kujua masuluhisho mbalimbali ya kifedha ikiwemo umuhimu wa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa wamenufaika na bidhaa za benki NMB na kushauri kuwa warsha kama hizo ziwe zinafanyika kila
mwaka angalau mara moja.

Leave A Reply