The House of Favourite Newspapers

NMB Yazindua Huduma Ya Kibenki Ya NMB KWETU Kwaajili Ya Diaspora Wa Kitanzania Waishio Nje Ya Nchi

0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi (wa pili kulia) akibonyeza kitufe kuzindua rasmi dirisha la huduma za kibenki kwa watanzania waishio nchi za nje (Diaspora) inayojulikana kama ‘NMB Kwetu’, huduma ambayo itawawezesha kujaza taarifa zote zinazohitajika kwa njia ya mtandao ili kufungua akaunti. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana (kulia), Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Mbelwa Kairuki.

Benki ya NMB imezindua huduma rasmi dirisha la huduma za kibenki kwa Watanzania waishio Nchi za Nje yaani Wana Diaspora inayojulikana kama NMB KWETU ambayo itawawezesha kufungua akaunti kwa mfumo wa kidigitali wa ukusanyaji wa nyaraka muhimu utakaowawezesha kufungua akaunti kwa njia ya mtandao.

Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na ushiriano wa Afrika Mashariki,Balozi Stephen Mbundi kwa niaba ya Waziri wa mambo ya nje na ushiriano wa Afrika Mashariki, Mh.January Makamba,mapema leo Septemba,29,2023, jijini Dar-es-Salaam ambapo amesema Wizara Yao ya mambo ya Nje na ushiriano wa Afrika Mashariki imekathimiwa jukumu kubwa la kuratibu na kusimamia masuala ya Watanzania wanaoishi Ughaibuni yaani Diaspora.

Amesema ameshukuru Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya NMB kwa uongozi makini unaojali wanafamilia wake popote walipo kuendelea kushirikia  na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha kuwa huduma ya sekta ya fedha inawafikia Watanzania popote walipo.

“Tumeshuhudia Serikali ya Awamu ya sita chini Raisi wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ikitambua mchango mkubwa ambao Diaspora wanao katika maendeleo ya Nchi yetu na kuwekeza nguvu kuwatambua na kuwawezesha kushiriki katika maendeleo ya Nchi yetu kwa namna mbalimbali,miamala wanayoileta kuchangia maendeleo lakini wamekuwa na mchango wa kuleta utaalamu wao.

Wageni waalikwa wakifuatilia matukio.

“Wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba huduma zinawafikia Watanzania ikiwemo za kijamii hasa katika huduma ya Afya,lakini Sasa hivi wanakwenda mbali wameamua hata kuacha mishahara na malupulupu makubwa wanayoyapata Ughaibuni wanakubali Sasa kuja kufanya kazi Serikalini.

“Mchango wa Diaspora wetu katika shughuli za uchumi umekuwa ukikuwa mwaka hadi mwaka na hili linathibitishwa na takwimu zilizololewa na Benki kuu ya Tanzania ambazo zinaonyesha kwamba katika kipindi Cha Januari hadi Desemba 2021 Diaspora wetu wametuma hapa Nchini fedha zaidi ya Dola milioni mia Tano sitini na tisa pointi tatu,na kwa mwezi Januari hadi Desemba 2022, jumla ya fedha ambazo zilitumwa ni Dola za Marekani bilioni 1.1 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Trilioni 2.6.

“Aidha katika mwaka 2022 uwekezaji ulifanywa na Diaspora wenye asili ya Tanzania kwa ununuzi wa nyumba na Viwanja kupitia shirika la nyumba la Taifa na mifuko ya hifadhi ya jamii ulikuwa ni shilingi bilioni 2.3 walizowekeza katika nyumba na Viwanja katika mwaka 2021,zaidi ya uwekezaji katika nyumba na viwanja.

Ameendelea kusema kuwa baadhi ya Diaspora wenye asili ya Kitanzania,wamekuwa wakiwekeza kwa  kununua hisa hapa Nchini na Leo imeelezwa Kuna benchi ambalo limeanzishwa na NMB na ana Imani wataichangamkia kwa haraka na kwa kasi kubwa.

Nae Afisa Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema wameanzisha huduma hiyo ya NMB KWETU ili kiwafungulia Wana Diaspora Duniani kwa kuwapa masuhuhisho mahususi ya kifedha.

“Huduma hii ya NMB KWETU akaunti tumeileta mahususi ambayo imetengenezwa kwa mfumo wa kidigitali wa ukusanyaji nyaraka utakaowawezesha Wana Diaspora kujaza taarifa zote zinazohitajika kwa njia ya mtandao ili kufungua akaunti.

“Mfumo huu utawawezesha wenzetu waliopo nje ya Nchi kuweza Kutuma nyaraka zote zinazohitajika kufungua akaunti ya NMB bila kuzisafirisha hizo nyaraka kwa njia ya kuzisafirisha kwa kawaida ama kwa kuzitumia kwa barua pepe, sisi tumekuwa kwa mfumo wa kidigitali ambao Sasa utarahisisha ukusanyaji wa hizo nyaraka na kwa hivyo ndugu zetu walipo nje ya Nchi waweze kufungua akaunti kwa urahisi kabisa bila kuhangaika kutuma hizo nyaraka sehemu mbalimbali ama kwa kutumia barua pepe ama kwa njia nyingine lakini pia hizi akaunti watazifungua hazitakuwa na makato yoyote.

“Kupitia huduma mahususi ya ‘NMB KWETU’ Wana Diaspora watanufaika na Bima ya maisha yenye dhamani ya hadi shilingi za Kitanzania milioni 29  bila gharama ya ziada kwa kushirikiana na kampuni ya bima Sanlam Life Insurance,pia hakutakuwa na makato ya mwezi yaani Monthly fees, kwa akaunti za Diaspora World Wide Pesa kwamba watatuma pesa nyumbani kwa ndugu,jamaa na marafiki kutoka Nchi zaidi ya 100 Duniani kwa kushirikiana na makampuni mahili ya Thunes na Terrapay.

“Fursa ya kupata mikopo ya nyumba (kununua ama kujenga) Fursa ya kuwekeza kwenye Amana za muda mfupi na Amana za muda mrefu zenye viwango shindani,kutumia huduma za kidigitali za Benki ya NMB kufanya miamala popote walipo Duniani.

Leave A Reply