The House of Favourite Newspapers

Nugaz -“Awaangukia Mashabiki, Tulieni Mambo Mazuri Yanakuja” -Video

0

Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema VIP A kitakuwa Sh 15,000 wakati VIP B na C kiingilio kitakuwa Sh 10000.

Nugaz amewataka mashabiki kufika kwa wingi katika mchezo huo utakaoanza saa 1:00 usiku ili kuiunga mkono timu yao huku akiwasisitiza kuzidi kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona kwa kuvaa barakoa.

 

“Maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanakwenda vizuri huku tukiamini tutapata ushindi.

“Niwaombe mashabiki waje kwa wingi uwanjani kuiunga mkono timu yao, najua kuna mambo mengi yametokea baada ya mechi na Azam na kupelekea baadhi kuwa na hasira na kuwashutumu wachezaji lakini niwaombe tuwe na subra na tuzidi kuwapa moyo wachezaji wetu ili tumalize mechi zilizobaki vizuri” amesema Nugaz.

 

Leave A Reply