The House of Favourite Newspapers

Nuh Mziwanda Alivyojichanga Kusimamisha Mjengo

DUSKODUSKO ni maneno maarufu kwa sasa mtaani, ambayo humaanisha fedha ndogondogo. Vijana wengi hupenda kulitumia pale wanapogawana, mtu anapojichanga kutunza fedha au kuomba aungiwe, utasikia anasema: “Niungie dusko mshikaji.” Akimaanisha apewe pesa kidogo.

 

Sasa kwa upande wa mastaa wengi Bongo, wao hutumia mamilioni ya fedha kusimamisha mijengo. Ni wachache ambao huweka wazi kuwa wamejichanga duskodusko na kusimamisha mijengo.

Kwa wanaokumbuka, mwaka 2015, wakati mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akihamia kwenye mjengo wake, Madale-Tegeta jijini Dar, alitangaza kwamba mjengo huo umemgharimu kiasi cha fedha za Kibongo zisizopungua shilingi milioni 280.

 

Na kwamba mjengo huo una bwawa kubwa la kuogelea, choo kilichonakishiwa kwa dhahabu iliyogharimu shilingi milioni 70, sehemu ya kufanyia mazoezi na michezo mbalimbali.

Diamond aliungana na wanamuziki kadhaa wakiwemo Profesa Jay, aliyewahi kutangaza kuwa anamiliki mjengo wa bei mbaya maeneo ya Mbezi ya Kimara, Dar uliyomgharimu zaidi ya shilingi milioni 100 kabla ya mwaka huu kupitiwa na bomoabomoa.

 

Hata hivyo, wanamuziki wengine wenye mijengo ya bei mbaya ni pamoja na Hamad Ally ‘Madee’ uliopo Mbezi ya Kimara na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ mwenye mjengo maeneo ya Kimara ambaye aliwahi kusema mjengo wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 180.

Lakini pia si hao tu, listi yao ni ndefu. Wachache ambao ninaweza kukuorodheshea hapa ni pamoja na Masanja, Joti na Mpoki ambao mijengo yao ya maana ipo maeneo ya Kigamboni, Dar.

 

Kuna Mr Blue, upo Tabata, Chege na Temba pamoja na wengine wengi.

Kama nilivyoeleza hapo awali wengi wa wasanii huitaja mijengo yao pale inapokamilika na kuonesha fahari za mijengo hiyo.

Jambo ambalo limekuwa tofauti kwa mwanamuziki Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambaye ameweka wazi namna anavyopata ugumu katika suala zima la ujenzi na kwamba anajichanga ‘duskodusko’, katika kuujenga. Huyu hapa Nuh akipiga stori na Over Ze Weekend;

 

Over Ze Weekend: Nuh mambo vipi, hongera kwa mafanikio, tunaona umepandisha mjengo…

Nuh: Mambo poa. Asante kwa pongezi, nimeamua kuonesha mjengo ili mashabiki wangu waone ninachokifanya kwa mchango wao katika kazi zangu. Pesa wanazotoa kwangu sizitumii vibaya.

Over Ze Weekend: Ni kawaida, wasanii wengi kuonesha mijengo yao pale inapokamilika, kwa nini wewe umeamua kuonesha kabla ya kuumaliza?

 

Nuh: Kwangu ni furaha kufika hapa ulipo, kwani nikiwa muwazi, kiukweli si rahisi kujenga. Na pale nimejichanga duskodusko ya pesa zangu ambazo nimekuwa nikipata kwenye shoo na kumtumia mama yangu.

Over Ze Weekend: Kwa hiyo bimkubwa ndiyo anasimamia ujenzi?

Nuh: Ndiyo, mama ndiye anasimamia mjengo, maana yupo karibu na ninapojenga huko Kivule (nje kidogo ya Jiji la Dar). Kwa hiyo kila ninachokipata ninamtumia, ananunua tofali, simenti au chochote kinacho-husika na ujenzi.

 

Over Ze Weekend: Mpaka sasa ume-tumia kiasi gani hadi mje-ngo wako ume-fikia hapo ulipo?

Nuh: Kama nilivyo-sema, nimeji-cha-nga dusko-dusko, kwa hiyo hesabu kamili ya kiasi gani nime-tumia hadi hapo mj-engo ulipofikia, kiukweli siwezi kufahamu, labda pengine mama yangu ndiye anayeweza kufahamu kwa kiasi fulani.

Over Ze Weekend: Ukipoachia picha za mjengo wako kwenye Instagram, uliandika kwamba ni kwa ajili ya mwanao, kivipi?

Nuh: Ndiyo, unajua nimeshakuwa mzazi. Kwa hiyo kila ninakichofanya kwa sasa si kwa ajili yangu peke yangu, ni kwa ajili ya familia yangu, hasa mwanangu na wapendwa wangu wengine akiwemo mama yangu.

 

Over Ze Weekend: Tukirudi kwa mzazi mwenzako, nini kinaendelea kati yenu?

Nuh: Hakuna zaidi ya kumuangalia mtoto.

Over Ze Weekend: Mmewahi kuzungumza kuhusu kurudiana?

Nuh: Hapana, kila mtu anaendelea na maisha yake.

Over Ze Weekend: Kwa hiyo sasa hivi una mpenzi mwingine?

Nuh: Mh! Mimi ni mwanaume, lolote linaweza kutokea, lakini kuzungumzia kuhusu hili suala ninahisi wakati wake bado, ukifika nitaweka wazi kila kitu.

 

Over Ze Weekend: Basi ninakushukuru Nuh, pengine kama una lingine lolote kwa ajili ya mashabiki wako?

Nuh: Lingine waendelea kunisapoti, kama nilivyowaonesha kile ninachopata kutokana na kazi yangu ninafanyia maendeleo na si anasa. Mungu awabariki sana! Pia wasikose kusoma Gazeti la Ijumaa Wikienda maana ndilo gazeti langu na linalopendwa na mastaa.

BONIPHACE NGUMIJE | IJUMAA WIKIENDA

Comments are closed.