The House of Favourite Newspapers

Nyakunyaku Wataka Kumpora Linah

0
Estalina Sanga ‘Linah’.

SEXY lady wa Bongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’ au ‘Ndege Mnana’ amefunguka kuwa amekuwa akikutana na vikwazo vingi kutoka kwa wanawake wenye tabia ya kupora waume wa wenzao, almaarufu nyakunyaku ambao wapo kwenye mitandao wa kijamii kwa ajili ya kuwanasa wapenzi wa wenzao.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Linah ambaye hivi karibuni alibahatika kupata mtoto wa kike na mchumba wake huyo aitwaye Shaban alisema kuwa, mara nyingi nyakunyaku wakiona mwanaume yupo na staa fulani, basi huwa wanatafuta kila mbinu waingie kwa Yule mwanaume waone kuna kitu gani anachofaidi staa huyo.

 

“Kikweli ninakutana na vitu vingi sana kutoka kwa mzazi mwenzangu, kuna wanawake wanamsumbua kwenye mitandao ya kijamii, wanataka kuona labda mimi nilipendea nini hivyo wanajaribu kila kona ili wanamnase ila wamegonga mwamba,” alisema Linah.

 

Mwanamuziki huyo aliendelea kufunguka kuwa, kikubwa alichokifanya ili kuwakwepa nyakunyaku ni kuwa na uhusiano na jamaa huyo ambaye hajulikani kabisa, lakini nyakunyaku wakizoea hawaangalii hilo.

 

“Sikutaka kabisa sasa hivi kutoka kimapenzi na mtu ambaye anajulikana, ndiyo maana nikaamua kuwa na mtu tofauti kabisa, lakini unajua nyakunyaku hawaachi ila nashukuru mtu wangu anawadharau,” alisema Linah.

Stori: IMELDA MTEMA, MWANZA

Leave A Reply