The House of Favourite Newspapers

NYAMA YA BUCHANI HAILALI!

Tokeo la picha la AFRICAN COUPLES ON BED

MAMA wa mashangingi wote mjini nimeingia, kungwi niliyepigwa mishale mingi, haloooo ehhhh na utachina mwaka huu! Shoga upo? Kama nakuona vile ukitamani kujua leo naongea nini. Weee naweee umbea umekujaa kama bomba la choo, hee heeeiyaaaa!  Leo nipo na nyie wanawake wenzangu mnaofanya hadi wote tuonekane mzazi wetu ni mmoja! Shoga kuna vitu vinaniwasha, jitu zima hoooovyoooo utakuta lichafuuu!

Nikisema uchafu shoga namaanisha, hivi mpaka lini tuonekane mbwa wa bosi, utakuta mwanamke kafuga mikucha kama anakwenda kupigana, huyohuyo ana mtoto mchanga, huyohuyo ndiyo hausigeli wa kumfulia na kumpikia kila kitu mtoto, jamaani!

Sawa kufuga au kubandika kucha ni urembo lakini inategemea unafuga hiyo mikucha nani akufanyie kazi nyingine, kwanza anayekufulia hayo makufuli yako ni nani na anayafuaje kwa mfano? loool!

Ndiyo maana kila siku najiuliza hivi hawa wanawake wengine mbona wanatukosea tukaonekana wote letu moja, mwanamke makucha hayo marefuu hajui matumizi yake zaidi ya kubadilisha siku tatu kabandua kaweka hizi kesho zile, hayo marangi ya kucha sasa utafikiri amepangwa kwenda kuimba wimbo wa taifa! Shuuutuuuu!

Shoga nina hasira, ujue mwanamke usafi na usafi wenyewe siyo kufua kufuli lako au kuweka uwanja safi, usafi wa nywele na mikucha yako! Siyo upo na babaa unaanza kumparua kama unaigiza muvi za kutisha, heee heeeiyaaa! Jicho langu miye nikifumba narembua, upo?

Mwanamke angalau ubakie na kucha chache shoga, mbili tatu vidole vya pembeni tena zile za kumchanganya mzee, unazitelezesha kwenye garden yake mpaka anajisahau anakupa hela ya gari badala akupe hela ya shopping! Ngoja nikung’ate sikio shoga yangu maana miye na wewe tena, kama dera na mtandio, shoga wanaume huwa wepesi kudanganywa kwa vitendo na muonekano sasa we shangaa kama mkulima aliyelima vitunguu akavuna nyanya.Picha inayohusiana

Mwenzangu tangu lini ukaona nyama ya buchani ikalala, wanaume wa sasa wajanja hawapendi kukaa na mwanamke asiyejielewa, hajui matumizi ya kucha kakalia kuyafuga kutwa anachana mashuka na ukiona mwanaume anakuvumilia na mikucha yako basi ujue kuna vitu kakupendea lakini ipo siku hatokuvumilia na kumtafuta mbadala wako.

Hivi kwanza kufuga hiyo mikucha vyombo unaoshaje kwa mfano? kupika sawa kufua je? tuachane na hayo huko msalani unafanyaje baada ya haja? Haloooo ehhhh tena ya kisoda anti fungua tuangalie zawadi.

Shoga maneno yangu kuntu, badilika mwenzangu, ni aibu tena kubwa kufuga mikucha hiyooo kisa urembo na kusahau usafi wako unategemea mikono hiyohiyo. Sitaki kuongea sana naomba niishie hapa, ni mimi Shangingi Mstaafu Anti Naa

Comments are closed.