The House of Favourite Newspapers

Nyasinski, Chameleon Na King Kiba Hapatoshi Kesho Oktoba Fest 2023 Coco Beach

0
Wakali wa muziki wa kizazi kipya Nyasinski, Kutoka nchini Kenya akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutua uwanja wa JNIA.

Dar es Salaam, 20 Oktoba 2023: Wakali wa muziki wa kizazi kipya Nyasinski, Kutoka nchini Kenya, Jese Chameleon kutoka nchini Uganda na King Kiba kesho wanatarajiwa kukisha jukwaa moja kwenye tamasha la Oktoba Fest 2023 linarotarajiwa kufanyika Ufukwe wa Coco jijini Dar.

Akizungumza baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mapema leo, Nyasinski amesema shoo itakuwa ni funga mwake kwake.

Meneja Mawasiliano na Uendelevuwa SBL, Rispa Hatibu mwenye fulana nyeupe akizungumza na Nyansiski na msafara wake baada ya kumpokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mapema leo.

“Hii ni shoo kubwa sana kwangu kufanyakazi jukwaa moja na wakongwe kama King Kiba na Chameleon hivyo name siwezi kufanya shoo ya kawaida isiyoacha historia ya kukumbukwa kwa balaa nikatakalolifanya”. Alisema msanii huyo maarufu kutoka Kenya.

Shoo iliyoandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kiingilio itakuwa ni bure unachotakiwa ni kufika kwenye Ufukwe huo.

Awali akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu SBL, Anitha Msangi Rwehumbiza alisema shoo hiyo itatawaliwa na radha na sauti za kitamaduni wa mtanzania zaidi ambapo wasanii kibao wanatarajiwa kusindikiza tamasha hilo.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply