The House of Favourite Newspapers

Nyati Spirit Tanzania Yazindua Vinywaji Vikali

0

????????????????????????????????????

Ofisa Habari wa Kampuni ya Nyati Spirit Tanzania, Alma Miraji akifafanua jambo kuhusu bidhaa zao mbele ya wanahabari (hawapo pichani).

Nyati Spirit Tanzania (2)
Viongozi wa Nyati Spirit Tanzania wakisikiliza maswali ya wanahabari (hawapo pichani).

Nyati Spirit Tanzania (5)Nyati Spirit Tanzania (4)

????????????????????????????????????

Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Mtaalamu akitoa maelezo ya utayarishwaji wa vinywaji hivyo.

KAMPUNI ya utengenezaji wa vinywaji vikali ya Nyati SpiritTz Limited ya jijini Dar, jana imezindua rasmi bidhaa zake mbili ambazo hivi karibuni zitaingia mtaani.

Akizungumza jana kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Uhakiki wa kiwanda hicho, Karan Suchak amesema  wamezindua bidhaa mbili ambazo ni DON NYATI na DUMA huku akibainisha kuwa kwenye pande wa  DUMA wana vinywaji kama LEMONQUILLA, MANGOQUILLA na COLAQUILLA wakati kwenye DON NYATI vipo HERITAGE na FUSION, kwa upande wa Heritage wana MAHALE WHISKY, MANYARA VODKA, MIKUMI GIN NA SELOUS BRANDY huku kwenye Fusion wakiwa na EMBE FUSION, KAHAWA FUSION, COLA FUSION NA TROPICAL FUSION.

“Tuna jumla ya vinywaji 11 na vinjwaji vyetu vina vilevi kama vinywaji vingine ila utofauti wetu ni kuwa vinywaji vya DON NYATI vina radha mbalimbali ikiwemo ya matunda, kahawa, embe na kadhalika,” alisema Suchak.

Hata hivyo Suchak amesisitiza kuwa vinywaji hivyo havitakiwi kutumiwa na mtu aliye chini ya miaka 18 na vitaingia mtaani muda wowote kuanzai sasa, Watanzania wavipokee kwani ni vya kipekee na vina ubora uliodhibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Leave A Reply