The House of Favourite Newspapers

NYIKA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA YANGA, ORODHA HII HAPA

WAAKATI kilabu ya Yanga ikiwa katika harakati kabambeĀ  kuelekea uchaguzi mkuu, jumla ya watu 28 mpaka sasa wamesharudisha fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Katika orodha ya majina hayo, jina la aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika limo katika orodha.

Ikumbukwe Nyika alitangaza kuachia ngazi hivi karibuni akiwaomba radhi wanachama na mashabiki wa Yanga kumsamehe kama kuna mabaya aliyafanya kipindi cha uongozi wake.

Comments are closed.