The House of Favourite Newspapers

Nyoni kuanza kazi Shinyanga

Erasto Nyoni (kushoto).

TAGETI ya kwanza ya Patrick Aussems ilikuwa kumrudisha uwanjani Erasto Nyoni katika mechi na JS Saoura wikiendi ijayo.

 

Lakini amebadili mawazo, kwenye mechi na Stand United kesho pale Shinyanga atampa shavu kidogo kumrudisha mchezoni. Ingawa amemuonya asizidishe mbwembwe asije kuumia tena.

Nyoni hajaonekana uwanjani tangu alivyumia kifundo cha mguu kwenye mechi ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu.

 

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 19, nyuma ya Azam FC nyenye pointi 50 na Yanga waliopo kileleni wakiwa nazo 61.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Nyoni alisema wazi kuwa kufuatia mwenendo wake mzuri kuanzia kwenye mazoezi, hana shaka ya kucheza mechi ya kesho kwani tayari ana utimamu wa mwili hivyo kama Mungu atajalia basi anaamini kocha atampa nafasi.

 

“Niko vizuri na nina imani nitakuwa sehemu ya mchezo wetu na Stand, maana hata kocha ameonekana kunisistiza sana kuongeza bidii kwenye mazoezi, hivyo kama Mungu akijalia naamini naweza kuanza au kuanzia benchi.

 

“Unajua kocha anajitahidi kila mchezaji acheze ili awe na utimamu kwa ajili ya mashindano yajayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Soura ya Algeria ambayo tunatarajia kusafiri baada tu ya kumalizana na huu mchezo wa Stand huku Shinyanga,” alisema Nyoni.

Stori: Musa Mateja, Dar es Salaam

Comments are closed.