DULLY AFURAHIA HARMONIZE ‘KUMKOPI’

MKALI wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amefunguka juu ya kutumiwa kwa melody ya wimbo wake wa muda mrefu unaofahamika kama ‘Handsome’ na msanii kutoka Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdul ‘Harmonize’ katika wimbo wake mpya alioutoa wa Kainama na kusema amefurahi kwa sababu ameona kama amemuenzi.  

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Dully alisema kabla Harmonize hajaweka maneno katika wimbo huo, alimshirikisha kwanza na hata wakati anarekodi alikuwepo studio na akamshauri baadhi ya vitu.

 

“Wala sijachukulia kama kaniibia melody yangu ila nimechukulia kama hali ya kunienzi f’lani hivi kwa nilichokifanya huko nyuma nilifurahi sana alipotoa wazo la kuchukua melody hiyo ambayo nilitumia katika wimbo wangu wa zamani uliokuwa unafahamika kama Handsome, na ameutendea haki vilivyo nimefurahi sana,” alisema Dully Sykes.

STORI: Shamuma Awadh

Toa comment