The House of Favourite Newspapers

Nyoshi Aja Kivingine!

0

MKALI wa Dansi Bongo ambaye ni Prezidaa wa Bendi ya Bogoss Musica, Nyoshi El Saadat amekuja kivingine ambapo anatarajia kuzindua staili mpya ya uchezaji baada ya kujizolea umaarufu na staili ya Naliamsha Dude.

 

Nyoshi ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, baada ya kutikisa jiji kwa staili hiyo kwa muda mfupi baada ya uzinduzi wa bendi hiyo, ameamua kuja na staili nyingine ambayo itakuwa gumzo zaidi ya Kuliamsha Dude.

 

“Nawaomba mashabiki wa burudani waje Guanzhou pale Tegeta- Kibo Complex (Dar), Agosti 2, mwaka huu. Nataka kuwadhihirishie mashabiki wa dansi kuwa kwa sasa sina mpinzani hapa Bongo.

 

“Nikiwa na kundi la wanenguaji wakali wakiongozwa na Queen Suzy na Salma Dallu tutaonesha mashabiki ladha mpya ambayo itawashika huku rapa Totoo Kalala, mkali wa kuchagiza akitia vionjo vyake kwenye staili hiyo,” amesema Nyoshi.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Leave A Reply