The House of Favourite Newspapers

Yusuf Mzee Kumwaga Kila Kitu Dar Live

0

NI miezi kadhaa imepita tangu atangaze kurejea mjini, Mzee Yusuf ambaye pia awali alikuwa Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, hatimaye Julai 30, mwaka huu ana jambo lake zito pale Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akistorisha na OVER ZE WEEKEND, mfalme huyo wa Taarab ambaye awali aliamua kumgeukia Mwenyezi Mungu hadi kufikia hatua ya kuwa Alhaj Mzee Yusuf amesema, watu wengi wanajiuliza anarudi mjini kufanya nini, lakini anaomba wawe wavumilivu kwani siku hiyo ndipo ataweka wazi kila kitu.

“Kurudi kwangu mjini kuna mambo mengi sana, kwa sababu wote tunajua kwamba mjini ndipo mambo mengi yalipo hivyo ukitaka kuwa sheikh haswaa unatakiwa uwe mjini, ukitaka kuwa mwizi kwelikweli ni mjini.

“Ukitaka kuwa msanii pia ni mjini, yaani wewe anzia popote utakapoanzia, lakini mjini ndipo kila kitu hivyohivyo na ukitaka kuwa mtangazaji mzuri lazima uwe mjini.

“Hivyo binafsi nimeona mjini kuna fursa, nimeona kuna kitu cha maana, kipo cha maana kwenye fursa, nilipohama mjini watu wengi walinipotea.

“Nimemkumbuka sana Fadha Mauji na Fatuma Nyoro, lakini sijamkumbuka sana RJ kwa sababu yeye huwa anakuja sana kijijini kwetu kunisalimia, hivyo watu wakae mkao wa kula mfalme wa muziki wa Taarab narudi mjini tarehe 30, mwezi huu pale Dar Live na ndiyo siku ambayo nitasema nimerudi mjini kufanya nini,” amesema Mzee Yusuf.

STORI: MEMORISE RICHARD

Leave A Reply