The House of Favourite Newspapers

Nyota wa Cameroon Atemwa Kisa VVU

0

Nlend

Samuel Nlend wakati akisaini mkataba na Klabu ya Al-Ittihad Alexandria ya Misri.

KLABU ya Al-Ittihad Alexandria ya Misri imetangaza kuvunja mkataba na nyota wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Nlend kutokana na kugundua kuwa nyota huyo ana HIV.

Samuel-Nlend

Samuel Nlend.

Al Ittihad Alexandria imevunja mkataba na Samuel Nlend mwenye umri wa miaka 21 kutokana na kupimwa kwa nyota huyo na kugundulika kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi, maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni siku nne zimepita toka nyota huyo asaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu hiyo.

Nlend 2

Samuel Agosti 24, 2016 alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea Klabu ya Al Ittihad Alexandria, Samuel amewahi kuichezea timu ya Taifa ya Cameroon mechi tano, hata hivyo hakuna sheria yoyote itakayomzuia staa huyo kupata kibali cha kucheza soka katika klabu nyingine licha ya kugundulika kuwa na virusi hivyo.

Leave A Reply