The House of Favourite Newspapers

Nyota wa Yanga Aibukia Zesco, Apishana na Kocha wa Yanga

0

DAVID MOLINGA, mshambuliaji wa zamani wa Yanga, anasemekana amejiunga na Klabu ya Zesco United ya Zambia iliyokuwa inanolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

 

Lwandamina aliibukia Zesco United baada ya kushindwana na mabosi wa Yanga kutokana na ishu ya malipo.

 

Wakati Molinga aliyekuwa mshambuliaji namba moja ndani ya Yanga ambapo alitupia jumla ya mabao 11 akiibukia Zesco, Lwandamina  ameachana na klabu hiyo.

 

Haijaelezwa sababu ya msingi ni ipi ya Lwanadamina kusepa ndani ya klabu hiyo kwani pande zote mbili zimekuwa kimya.

 

Wakati anaondoka,  Zesco iko nafasi ya tano katika msimamo ikiwa na pointi 47 wakati vinara wa Ligi Kuu Zambia, Nkana,  wana pointi 50.

Leave A Reply