The House of Favourite Newspapers

Mukoko, Chama Ndani ya Vita Mpya

0

VITA ya ufalme ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa inazidi kushika kasi ambapo nyota watatu kutoka Yanga na Simba wanapambana kuuteka ufalme uliopo mikononi mwa Clatous Chama wa Simba ambaye ni mchezaji bora kwa msimu wa 2019/20.

 

Ikiwa kwa sasa ni mzunguko wa tatu tayari timu zote zimecheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 na vita kubwa imeanza kuonekana kwa nyota wapya na wale waliokuwa na vikosi hivyo kwa msimu uliopita.

 

Kwenye hii vita, Chama ndiye ameshika usukani kwa kuwa amehusika kwenye mabao manne kati ya saba ambayo yamefungwa na timu yake na msimu uliopita alihusika kwenye mabao 12 kati ya 78 baada ya kufunga mabao mawili na kutoa pasi 10 za mabao.

Hiki ndicho alichofanya Chama akiwa ametumia dakika 270, alianza mbele ya Ihefu ambapo aliyeyusha dakika 90 alitoa pasi moja ya bao Uwanja wa Sokoine, Uwanja wa Jamhuri mbele ya Mtibwa Sugar pia aliyeyusha dakika 90 pamoja na mchezo wake wa tatu mbele ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao Luis Miqussone, kiungo mshambuliaji ndani ya Simba ametumia jumla ya dakika 180, akicheza mechi mbili alianza ile dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri na ya pili ilikuwa dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikishinda mabao 4-0 alipiga ‘hat trick’ ya asisti.

 

Chris Mugalu, ingizo jipya ndani ya Simba limetumia dakika 14 na kupachika bao moja kati ya saba ambayo yamefungwa na timu yake ilikuwa mbele ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 alichukua nafasi ya Meddie Kagere aliyefunga pia bao moja.

 

Kwa upande wa Yanga wao wanaye Tonombe Mukoko, ingizo jipya kutoka AS Vita ya Congo ambaye ametumia dakika 195 ilikuwa dakika 15 mbele ya Tanzania Prisons, 90 mbele ya Mbeya City na 90 mbele ya Kagera Sugar ambapo alifunga moja.

 

Michael Sarpong ingizo jipya kutoka Klabu ya Rayon Sports mbele ya Tanzania Prisons, Mbeya City na Kagera Sugar aliyeyusha kote dakika 90 na kumfanya atumie dakika 270 huku akipachika bao moja mbele ya Prisons Uwanja wa Mkapa. Mwingine ni Tuisila Kisinda ambaye ametumia dakika 225 ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons dakika 45, Mbeya City 90, na Kagera Sugar 90 alitoa pasi moja mbele ya Kagera Sugar.

Stori; Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply