The House of Favourite Newspapers

‘Nyota ya Yesu’ Yaonekana Live Bethlehem

0

BAADA ya zaidi ya miaka 400, jana (Jumatatu) usiku sayari mbili kubwa zaidi katika mfumo wetu wa jua, sayari ya Jupita au Mshtarii (Jupiter) na Zohali (Saturn) zilionekana katika umbo moja kutoka duniani.

Tukio hili ambalo hutokea mara moja katika muda wa uhai wa mwanadamu linafanya sayari hizo mbili kuonekana kama ‘nyota’ moja.

Kioja hicho kimewafanya wanajimu na walimwengu waliokishuhudia kukitaja kama ‘Nyota ya Yesu’ ambayo waliishuhudia live (mubashara) sehemu mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na Bethlehem.  Hii ni pamoja na kutokea wakati wa sasa ambapo ni ‘ukingoni’ wa sherehe za Krismasi.

Mara ya mwisho tukio kama hilo kuonekana ilikuwa zaidi ya miaka 400 iliyopita, Julai 16 mwaka 1623.

 

Si kweli kwamba sayari hizo mbili zitaungana na kuwa kitu kimoja, kuna umbali wa zaidi ya kilomita 733,205 kati ya sayari hizo mbili, na umbali wa kilomita 886,440 kati ya dunia na sayari ya Zohali, ila sayari zote mbili zitakuwa katika mstari mmoja wa mwonekano kutoka duniani ambapo wataalam wanauita ‘Muunganiko Mkuu au Mkubwa’ (Great Conjunction).

Sayari hizi mbili kubwa zinaonekana kwa urahisi kutoka duniani, na tukio hili linaweza kuonekana katika maeneo mengi duniani. Tafuta sehemu nzuri usiku wa leo utazame upande wa Kaskazini Magharibi uweze kuona tukio hili ambalo hautaweza kuliona tena katika maisha yako.

 

Mazingira ya muunganiko huo yanaonekana kuwa karibu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 800 iliyopita.  Ni muunganiko huo uliozaa Nyote ya Bethlehem, au Nyota ya Krismasi, ambao uliwavuta mamajusi watatu kutoka Mashariki kwenda  kumtembelea mtoto Yesu kufuatana na simulizi za Biblia.

Hili limo katika simulizi ya Kuzaliwa kwa Yesu katika Injili ya Mathayo ambapo mamajusi hao walimwuliza Mfalme Herode, “ni wapi Mfalme wa Wayahudi alipozaliwa kwani tumeiona nyota yake Mashariki na tumekuja kumsujudia.”

Inasemekana nyota hiyo iliwaelekeza hadi nyumbani kwa mtoto Yesu ambako walimsujudia na kumpa zawadi za dhahabu na manukato.

Tukio hili linatarajiwa kujitokeza zaidi wakati wa Sikukuu ya Krismasi mwaka huu (2020).  Hii ni pamoja na habari za kinajimu za China na Korea kusimulia kuhusu nyote iliyowahi kuonekana angani mnamo miaka mitano Kabla ya Kristo na ambayo ilidumu angani kwa siku 70.

Wanajimu wa zamani wamekuwa wakiandikakuhusu nyota ‘kuning’inia’ katika miji kadhaa kama Nyote ya Bethlehem ilivyosemekana kusimama juu ya eneo alipozaliwa Yesu katika muji huo.

Muunganiko huo unavyoonekana angani wa sayari hizo, hutokea kila baada ya miaka 20, lakini wakati wa mwisho zilikaribiana zaidi mwaka 1623 lakini kioja hicho hakikuonekana duniani.

Mwonekano wa mwisho ulionekana kwa vifaa vya ‘telescope’ mwaka 1226 wakati wa ujenzi wa Kanisa la Notre Dame huko Paris, Ufaransa.

 

Sayari hizo mbili zimekuwa zikisogeleana katika anga la kusini-kusini-mashariki kwa wiki kadhaa.

Mng’ao huo wa sayari mbili hizo umeibua hisia za wazi kuhusiana na ‘Nyota ya Krismasi’ inayotajwa katika Agano Jipya kuhusu mamajusi na Mtoto Yesu.

 

Muunganiko Mkuu mwingine wa sayari hizo mbili utatokea Novemba 2040.

Na kioja kinachofanana zaidi na cha Jumatatu kitatokea tena mnamo Machi 2080, na kujiokeza kwa ukaribu zaidi tena miaka 337 mnamo Agosti 2417.

Leave A Reply