Washington (CNN): Rais Barack Obama ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma za udukuzi zilizofanywa na nchi ya Urusi katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika Novemba 8 mwaka huu ambapo bwana Donald Trump wa Chama cha Republican aliibuka mshindi kwa kumbwaga mpinzani wake, Bi. Hillary Clinton.
Trump na Obama.
Rais Obama ameyasema hayo jana kwenye Ikulu ya nchi hiyo ‘White House’ kufuatia ripoti iliyotolewa na Central Intelligence Agency (CIA) ikieleza kuwa, nchi ya Urusi iliingilia mfumo wa Kompyuta wa Tume ya Uchaguzi ya Marekani unaotumika kuhesabu matokeo hivyo kuuharibu kwa lengo la kumsaidia bwana Trump kushinda uchaguzi huo ambapo inasemekana tukio kama hilo lilifanyika kwenye uchaguzi wa nchi hiyo mwaka 2008.
Viongozi wa Tume ya Uchaguzi wa nchi hiyo wamesema kuwa, endapo itabainika kuwa mfumo huo ulidukuliwa na Warusi, basi kura zote zitarudiwa kuhesabiwa upya na matokeo yatatolewa kabla ya Januari 20 ambapo bwana trump anatarajiwa kuapishwa.
Kwa upande wa Urusi wamekanusha kuhusika na udukuzi huo huku Wizara ya Mambo ya nje ya nchi hiyo ikiitaka Marekani ithibitishe iwapo kweli walidukua mfumo wa kompyuta wa uchaguzi wa Marekani. Waziri wa Mambo ya ndani wa Urusi amesema ni mara kadhaa wamewaeleza Marekani kutoa uthibitisho lakini wameshindwa kufanya hivyo.
Comments are closed.