The House of Favourite Newspapers

Ofisa Chama cha Waajiri Alipiga ‘Tafu’ Kanisa la EAGT

0

1. 2

Mkuu wa Masasiliano na Masoko wa Chama cha Waajiri Tanzania, Joyce Nangai, akifafanua risala aliyosomewa katika hafla hiyo

3 Shughuli ya harambee ikiendelea kanisani hapo.

4 Baadhi ya waumini wa kanisa wakifuatilia hafla hiyo.

5. Nangai (kulia) akimkabidhi shilingi milioni moja mmoja wa viongozi wa kanisa hilo.

6 Wakipeana mkono baada ya makabidhiano hayo.

7 Nangai akiungwa mkono na baadhi ya wageni waalikwa kwa kuchangia harambee hiyo.

NA DENIS MTIMA/GPL

MKUU wa Masasiliano na Masoko wa Chama Cha Waajiri Tanzania, Joyce Nangai, jana alichangia Sh. Milioni 5, kwa Kanisa la Ebeneza Christian Centre (EAGT) linalomilikiwa na Mchungaji Lukas Kimila lililopo Yombo-Vituka jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ilifanyika jana wakati Nangai alipokuwa mgeni rasmi wa uchangiaji  shughuli hiyo  ya harambee iliyofanyika kanisani hapo kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa kanisa hilo linalokadiriwa kugharimu kiasi cha Sh. Milioni 200.

Akizungumza katika hafla hiyo, Nangai alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kushiriki shughuli hiyo ya uchangiaji fedha za malengo ya kupanuzi sehemu ya utoaji huduma wa Neno la Mungu.

“Mimi na familia yangu kwa kuona hilo tutachangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa nyakati tofauti lakini leo nitatoa shilingi milioni moja tu,” alisema Joyce.

Leave A Reply