The House of Favourite Newspapers

Okwi, Niyonzima wafunika Simba Day

0
okwi niyonzima wafunika simba
Niyonzima

NYOTA wapya wa Simba, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Aishi Manula, jana walifunika kwa kushangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa timu hiyo wakati wakitambulishwa kwao.

 

Simba, jana ilifanya Tamasha la Simba Day ambalo hufanyika kila mwaka kabla ya kuanza kwa msimu likiwa na lengo la kutambulisha wachezaji watakaotumika msimu mzima na utambulisho wa jezi pia. Katika tamasha hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa umati wa mashabiki, Simba iliwatambulisha wachezaji wake wote wapya na wa zamani lakini Okwi, Niyonzima na Manula ndiyo walioshangiliwa sana.

 

Mshereheshaji katika utambulisho huo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alipoanza kutaja jina
la mchezaji mmoja mmoja kati yao, alikumbana na kelele nyingi za ushangiliaji kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.

 

Alianza kumtambulisha Manula aliyesajili kutoka Azam FC ambako alimaliza mkataba, kipa huyo alishangiliwa kwa nguvu, akafuatia Okwi aliyesajiliwa kutoka SC Villa ya Uganda kisha akamalizia Niyonzima aliyetokea Yanga.

okwi niyonzima wafunika simba
OKwi

Hata hivyo, Okwi na Niyonzima ndiyo waliofunika zaidi kwa kushangiliwa na mashabiki wengi waliojitokeza uwanjani hapo. Wachezaji wengine waliotambulishwa jana ni Method Mwanjale, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’, Mwinyi Kazimoto, James Kotei, Shiza Kichuya, Laudit Mavugo, Mohammed Ibrahim, Juma Liuzio, Paul Bukaba, Jamal Mwambeleko, Erasto Nyoni, Emmanuel Mseja, Said Mohammed ‘Nduda’, Ally Shomary, Yusuph Mlipili, Salim Mbonde, Manula, Shomary Kapombe, Said Ndemla, John Bocco, Nicholaus Gyan, Okwi na Niyonzima

Na: Omari Mdose| CHAMPIONI JUMATANO| DAR ES SALAAM

Leave A Reply