The House of Favourite Newspapers

Ombi la Mbowe na Wenzake Lakataliwa Mahakamani

0

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imekubali pingamizi la mawakili wa Serikali la kutopokea barua kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya ugaidi inayomkabili Mwenyeki wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

 

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Novemba 29, 2021 na Jaji Joachim Tiganga na kueleza kuwa mshtakiwa huyo Mohamed Ling’wenya hajaweza kuieleza mahakama ni kwa nini barua hiyo inamhuri wa naibu msajili.

Jaji ameeleza kuwa katika mazingira hayo mahakama imeshindwa kuelewa kama hiyo barua aliyotaka kuitoa ndio hiyo iliyopelekwa kwa RPC.

 

Jaji Tiganga ameingia na kesi inaitwa na karani

Mawakili wa Serikali wanatambulishwa na kiongozi wa jopo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando

Mawakili wa utetezi saa wanatambulishwa na kiongozi wa jopo, Peter Kibatala.

Jaji anawaita washtakiwa mmoja mmoja kwa namba nao wanaitika.

 

Wakili wa Serikali Kidando: Mheshimuwa Jaii shauri hili linakuja kwa ajili ya ruling, na tuko tayari

Kibatala: Na sisi Mheshimiwa Jaji tuko tayari kupokea ruling pamoja na kuendelea kadri Mahakama itakavuoelekeza

Jaji Tiganga: Mahakama imeandaa maamuzi na haya ndio maamuzi yenyewe. Kwa kuwa maamuz ni marefu nitasoma maeneo muhimu lakini hoja zote zimezingatiwa.

 

Sasa Jaji Tiganga anaanza kusoma uamuzi kwanza akifanya muhtasari wa chimbuko la pingamizi na hoja za pande zote, kabla ya kufanya uchambuzi wake na hatimaye kutoa hitimisho kama pingamizi linakubaliwa au linatupiliwa mbali.

 

Jaji Tiganga: Kuhusjana na unique feature za kielelezo (barua) mahamama imeridhika kuwa shahidi (mshtakiwa) ameweza kuzitaja ambazo ni uwepo wa sahihi ya wakili, jina lake shahidi (mshtakiwa) na mhuri wa Mahakama. Hivyo mahakama imetupiliabmbali hoja ya kwanza ya pingamizi.

 

Sasa Jaji Tiganga anajadili hoja ya pili: Pingamizi la Serikali linalohusu Chain of custody (mnyororo wa uhofadhi wa kielelezo).

Shahidi hajaweza kueleza akioneshwa. Na wakili wake barua hiyo wapi na lini na ni muda gani ameweza kuutumia kuwa na uelewa na kielelezo hicho na kwamba amekutana nacho katika mazingira gani mpaka aweze kukitoa mahakamani.

 

Mahakama ya Rufani ilishaweka wazi kuwa moja ya kigezo shahidi kutoa kielelezo ni kuwa na uelewa kuhusiana na kielelezo hicho.

Katika haki hiyo na kubakiana na upande wa Jamhuri kuwa shahidi alitakiwa aonyeshe kuwa ana uelewa wa kielelezo na alitakuwa alifanye hilo wakati akitoa ushahidi.

 

Kuonyeshwa tu kielelezo bila ushahidi kuwa amekimiliki ni jambo ambalo haliko kisheria.

Pia hajaeleza baada ya kuoneshwa kielelezo hicho alikifanyia nini kama aliona content.

Hivyo mahakama inashindwa kuamini kuwa shahidi huyu ana uelewa wa kielelezo hicho

Lakini pia katika eneo hilo barua hiyo imeelekezwa kwa Kamanda wa Polisi Ilala na nakala kwa mshtakiwa na kwa Naibu Msajili.

 

Ni kweli nyaraka iluyoombwa kutolewa hapa mahakamani ni barua iliyoandikwa kwa Kamanda wa Polisi Ilala.

Nakubaliana shahisldi akipewa nakala na pale mtoa nyaraka anapotoa nakala kwa mtu mwingine anakuwa analenga kuwa imfikie.

Hata hivyo kuna kigezo na moja lazima huyo aliyepewa aseme aliipokea na lazima atoe hiyo aliyopewa.

 

Lakini nyaraka aliyooneshwa shahidi tayari ilikuwa na mhuri wa Msajili, katika mazingira hayo nakala anayotaka kuitoa si nakala yake maana yake isingekuwa na mhuri bali anataka kutoa nakala iliyopelekwa kwa Msajili.

Shahidi hajasema ilikuwaje ikamfikia yeye.

Hivyo shahidi hajaweza kuiambia mahakama ni kwa nini barua anayotaka kuitoa ina mhuri wa Naibu Msajili.

 

Katika mazingira hayo mahakama inashindwa kuelewa kama hii anayotaka kuitoa ndio hiyo iliyopelekwa kwa RPC

Katika mazingira hayo mahakama inaona shahidi ameshindwa kuthibitisha chain of custody hivyo inakikataa kielelezo hicho.

Baada ya uamuzi huo sasa shahidi huyo wa kwanza wa utetezi katika kesi ndogo (mshtakiw Ling’wenya) anaendelea na ushahidi wake.

 

Kwanza Jaji anamkumbusha shahidi kuwa bado yuko chini ya kiapo.

Kisha Wakili wake Dickson anaendelea kumuongoza kutoa ushahidi wake.

Shahidi: Mimi Central Dar sijafika ndio maana nikamuomba Kamanda kuwa aweze kutoa uthibitisho kuwa shahidi huyo (wa pili upande wa mashtaka) alinipokea Central tarehe 7, 2020 maana mimi tarehe hiyo 7, 8 na 9 nilikuwa kituo cha Polisi Tazara.

 

Kwenye ile selo niliyokuwepo (Tazara) kulikuwa na mahabusu wengi na sikupata muda wa kuingia kuongea nao.

Wakili Matata: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Shahid amemaliz ushahidi wake wa msingi na sasa anahojiwa na kwanza mawakili wa washtakiwa wengine kisha watafuata upande wa mashtaka.

Anaanza wakili wa mshtakiwa wa kwanza (Halfan Bwire) wakili Nashon Nkungu:

Wakili: Ulisema ulikuwa inachukuliwa video, nani alikuwa anakuchukua video?

 

Shahidi: Nilichukukuwa video Moshi na Tazara, aliyenichukua Moshi ni tofauti na wa Tazara ambaye simfahamu.

Wakili: Ni wakati wa tukio gani ulikuwa unachukuliwa video?

Shahidi: Moshi ilikuwa wakati napigwa na Tazara wakati nahojiwa

Wakili: Unafahamu kwamba ni takwa la kisheria ukihojiwa kuchukuliwa video?

Shahidi: Nimekuja kujulia hapa Mahakamani

Wakili: Umeziona hapa mahakamani hizo video zikitolewa?

 

Shahidi: Hapana sikuziona

Wakili: Unafahamu ni takwa la kisheria mtuhumiwa kufikishwa mahakamani mara moja?

Shahidi: Nafahamu

Wakili: Unafahamu mara kadhaa DPP ametoa mwongozo mtu asifikishwe mahakamani mpaka upelelezi ukamilike?

Shahidi: Ndio Nafahamu

Wakili: Wewe ulikamatwa lini?

Shahidi: Tarehe 5/8 /2020

Wakili: Ulifikishwa lini Mahakamani kwa mara ya kwanza?

 

Shahidi: Tarehe 19/8/2020

Wakili: Iliikuwa ni baada ya siku ngapi?

Shahidi: Siku 14

Wakili John Mallya: Ulipokamatwa Moshi cha kwanza kufanyiwa ni ninj?

Shahidi: Nilipelekwa kwenye chumba cha mateso

Wakili: Ni kitu gani shahidi uhijisi ni chumba cha mateso?

Shahidi: Nilikutana na rungu, chuma na kamba.

 

Wakili: Ulikuwa katika hali gani?

Shahidi: Nilikuwa nimefungwa pingu mikono, ile kamba nikafungwa miguu, bomba kikapitishwa katikati ya miguu na mikono wakainua

Wakili: Ukawa katika hali gani wakati huo?

Shahidi: Nikawa kama popo naning’inia

Wakili: Watu gani hao wakihusika kukufanya uning’inie?

Shahidi: Upande mmoja alishika Jumanne, upande mwingine Goodluck na Mahita ndio alikuwa ananipiga na rungu

Wakili: Mahita alikupiga sehemu gani?

 

Shahidi: Wakati huo Kingai alikuwa wapi?

Shahidi: Yeye alikuwa amesima a tu pembeni

Wakili: Hilo zoezi la kukupiga kwenye nyayo lilichukua mudu gani?

Shahidi: Lilichukua kama nusu saa

Wakili: Walikuwa wanakuuliza nini?

Shahidi: Kwamba umekuja kufanya nini Moshi?

Wakili: Uliwajibuje?

 

Shahidi: Kwamba nimekuja kwa ajili ya VIP Protection kwa Mheeshimiwa Mbowe, wao walikuwa wanakataa kwamba sisi tunajua tulichokuja kufanya

Wakili: Nani alikuwa anauliza?

Shahidi: Alikuwa anauliza mmoja lakini wengine wanadakia kuwa siyo kweli, sisi tunajua

Wakili: Baadye kilitokea nini?

Shahidi: Nilisikia sauti ya mtu kuwa muacheni

Shahidi: Ilikuwa ya nani?

 

Shahidi: Sijui lakini kama alikuwa askari

Wakili: Nini kilifuata?

Shahidi: Nilifunguliwa nikarudishwa mahabusu

Wakili: Lini ulifunguliwa pingu?

 

Shahidi: Nilifunguliwa pingu tarehe 19/8/2020 mahakamani Kisutu

Wakili: Kuna watu wengi hapa wamekuja wakasema baada ya kukamatwa mlikwenda sijui kuwatafuta watu gani?

Shahidi: Ni uwongo

Wakili: Kuna huduma gani za kijamii?

Shahidi: Pale Moshi mimi sikupewa chakula

Wakili: Sasa nakuja safari ya Dar, nani alikutoa mahabusu?

 

Shahidi: Goodluck na Mahita.

Wakili: Ulikuwa katika hali gani?

Shahidi: Nilikuwa nimeinamishwa shingo, baadaye nikamuona Adamoo naye analetwa, akaingizwa kwenye gari kisha nikafungwa kitambaa kizito usoni.

Wakili: Lengo lao lilikuwa nini?

Shahidi: Labda walitaka nisione napelekwa wapi.

 

Wakili: Mikono ilikuwa katika hali gani?

Shahidi: Ilikuwa imefungwa pingu

Wakili: Safari yako ilikuwaje? Luxury au ya namna gani?

Shahidi: Ilikuwa ya mateso maana nilikuwa nimeinamishwa tu shingo na kufungwa kitambaa.

Wakili: Ni nini kilikufanya uone ni mateso?

Shahidi: Kulingana na vitendo nilivyokuwa nafanyiwa

 

Wakili: Mliondoka saa ngapi?

Shahidi: Jioni na tukafika alfajiri Dar

Wakili: Kwa masaa hayo uliyokuwa njiani kuna huduma yoyote ya kibinadamu ulipata?

Shahidi: Hakuna huduma ya kibinadamu nilipata

Wakili: Chakula?

Shahidi: Sikupata chakula hadi waliponifikisha Tazara

 

Wakill: Wale wasafirishaji wako walikwambia ni Tazara?

Shahidi: Hapana, mlango ulifunguliwa tu nikashushwa nikiwa nimefungwa kitambaa, nikaingizwa selo

Wakili: Kilichokusaidia kujua mlango umefungululiwa ni nini?

Shahidi: Nilisikia tu kwa masikio

 

Wakili: Pale Tazara kutuoni kuna mahali uliandikishwa?

Shahidi: Mimi sikuandikishwa popote nilipitishwa tu mpaka mahabusu

Wakili: Mikono ilikuwaje?

Shahidi: Ilikuwa bado imefungwa pingu

Wakili: Ulisema baadaye ulihamishiwa kituo cha Mbweni, hali ilikuwaje?

Shahidi: Bado nilikuwa nimefungwa pingu na kitambaa.

Wakili: Njiani ilikuwaje?

 

Shahidi: Nilikuwa natishwa kwamba ukicheza tutakupoteza kama Lujenge kule Moshi, halafu Goodluck alikuwa ananichomachoma kwenye mbavu na kitu kama bastola

Wakili: Kwa nini ulihisi ni bastola?

Shahidi: Maana Goodluck muda mwingi alikuwa ameshika bastola.

 

Wakili: Ulisema baadaye akaja Jumanne na maelezo akakulazimisha kusaini, ulikuwa katika hali gani?

Shahidi: Niliogopa maana Goodluck alikuwa amesimama mlangoni na bastola anakasema ukileta janjajanja tutakufanya kama Moshi.

Wakili: Nilikusikia ukiwataka wanajeshi wengine hapa, hao ushiriki wao ukikuwaje katika hili?

Shahidi: Nlikutana nao tu kwa mara ya kwanza Tazara wakaniambia usihofu hapa ni Tazara sasa labda walitaka kuhakikisha kuwa na mimi nimetoka JWTZ.

Leave A Reply