The House of Favourite Newspapers

Ommy Dimpoz Afunguka Sakata la Baba Yake, Aeleza Kila Kitu “Hakuja Kumzika Mama”-Video

0
Faraji Nyembo ni baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Omary Faraji Nyembo almaarufu Ommy Dimpoz ambaye ameonesha kuchukizwa na kile kinachoendelea mitandaoni kuhusu baba yake huyo

 

Baba wa Ommy Dimpoz amezungumza mambo mengi na vyombo vya habari kuhusu uhusiano wake na jamaa huyo akisema wana mawasiliano mazuri huku akipuuzia mbal madai kwamba mwanawe huyo amemtelekeza.

 

Sasa; baada ya mahojiano ya baba yake, Dimpoz amejitokeza hadharani na kufunguka mazito huku akifafanua kwamba mzee wake huyo ameendelea kung’ang’ania kwamba yeye ni baba mzazi wa Ommy Dimpoz na haambiwiki kitu juu ya hilo.

 

Hata hivyo, kinachomshangaza Dimpoz anasema kuwa, hajawahi kuwa karibu na baba yake huyo kwa sababu hakuwahi kumlea na hata mama yake mzazi alipofariki dunia, hakwenda kumzika.

 

Ommy Dimpoz anasema; “Nimekua nikilelewa na mama yangu, nilipokuwa primary, mama yangu alifariki. Katika msiba wa mama yangu, baba sikumuona, hakuja hata kunipa pole, lakini yule mtoto aliyekuwa hathamini ndiye amekuwa kimbilio.


“Baba yangu ana watoto zaidi ya 14, lakini anachotaka kuitwa Baba Dimpoz, wakati mimi ni mtoto wan je ya ndoa.

 

“Mara ya mwisho kukutana naye ni zaidi ya miaka 20, akaniambia ana watoto wengi, akasema wakikuwa watamtafuta baba yao….”

STORINA SIFAEL PAUL | GPL

Leave A Reply