The House of Favourite Newspapers

Ommy Dimpoz ajigonga kwa Shwomeley wa La Musica Band

0

ommy (1)Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’

Boniphace Ngumije

IMEVUJA! Msanii mwenye jina lenye uzito katika anga ya Muziki wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ameonesha kujigonga kwa mwanadada mwenye sauti mwanana kutoka kundi linalofanya muziki wa dansi nchini, La Musica Vijana Classic Band, jambo lililoonesha kuwa huenda wawili hao wakaishia kwenye ulimwengu wa malovee.

Akichonga mbili-tatu na mwandishi wetu, Leila Abdallah ‘Showmeley’ alisema Dimpoz alianza kuonesha kuvutiwa naye baada ya yeye kumtafuta kupitia mitandao ya kijamii kwa ajili ya ishu za kimuziki na baada ya kupata namba yake wamekuwa wakiwasiliana kila mara huku Dimpoz akiwa wa kwanza mara nyingi kumtumia ujumbe wa maandishi ‘sms.’

“Sina uhakika moja kwa moja kama moyoni mwake anawaza kuhusu uhusiano wa kimapenzi, lakini ukweli ni kwamba inaonekana ametokea kuvutiwa sana kuwasiliana na mimi maana kila mara huwa ananitumia sms,” alisema mwanadada huyo.

Gazeti hili lilikwenda mbele kwa kumvutia waya Dimpoz ili azungumzie hii ishu lakini simu yake haikuweza kupatikana mpaka tunakwenda mitamboni.

Leave A Reply