The House of Favourite Newspapers

Yanga yashtuka, yabadili gia angani

0

PluijmKocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm.

Wilbert Molandi
Dar es Salaam
UKIPATA nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Yanga, kazi yako ni moja tu kupokea pasi na kutoa mpira kwa mwenzako basi, hakuna mbwembwe zaidi. Ukibisha utakaa benchi.
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema hakuna jinsi kwani timu yake ndiyo inayoongoza kwa kukamiwa katika mechi zake na kama akiendelea kuwaachia wachezaji wake kuweka ufundi mwingi itakula kwao.

kocha-wa-yanga-hans-van-der-pluijm-kulia-na-msaidizi-wake-juma-mwambusi_ljoz3t1bxy5u1wsl6o34xdnmmHans van Der Pluijm akiongea jambo na kocha msadizi wake Juma Mwambusi.
Pulijm raia wa Uholanzi ambaye kesho Jumapili timu yake itacheza na Ndanda FC katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, alisema; “Nashangaa, timu zikicheza zenyewe zinacheza hovyo, lakini zikija kwa Yanga ni hatari na zinakamia kama fainali.

YANGA (2)Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi.

“Haya ndiyo yanayozikuta timu kubwa siku zote kote duniani, sasa na mimi nimebadili mfumo wa uchezaji na mbinu kwani mchezaji anatakiwa kutoa pasi haraka pindi anapopata mpira.
“Nataka wacheze pasi za haraka ambazo hazitawapa nafasi wapinzani kupokonya mpira hata kujipanga zaidi na kuleta madhara kwetu, naamini tukicheza hivyo tutabadilika na kuwa wazuri zaidi.”

YANGA (3)

Akizungumza na Championi Jumamosi, Pluijm alisema kuwa aina ya soka analolitaka hivi sasa ni lile linalofanana na la pasi za haraka kama zinavyocheza Barcelona ya Hispania na Arsenal ya England.
Pluijm alisema; “Aina hii ya uchezaji itawaepusha wachezaji kugongana na wapinzani wao ambao kila siku hutuchezea soka la kupania.”
Yanga imerejea katika ligi kuu baada ya kutoka Zanzibar ambako ilikuwa ikishiriki Kombe la Mapinduzi na kuishia hatua ya nusu fainali kwa kutolewa na URA ya Uganda ambayo ilitwaa ubingwa baadaye.
Ikimaliza mechi yake na Ndanda kesho, Alhamisi ijayo uwanjani hapo Yanga itacheza na Majimaji ya Songea katika muendelezo wa ligi hiyo.

Leave A Reply