The House of Favourite Newspapers

Omog: Tupo tayari Ligi Kuu Bara

2

pic+omog Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog.

Wilbert Molandi,Dar es Salaam

WAKATI timu yake ikijiandaa kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, leo Jumamosi, Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, ametamba kuwa kikosi chake kimeiva na kipo fiti kwa ajili ya ligi.
Simba inatarajiwa kufungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa kuvaana na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Omog alisema ana matumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mechi yao na Ndanda, hiyo ni kutokana na maandalizi aliyoyafanya.
“Ninaweza nikatamka kuwa, kikosi changu kimeiva hivi sasa, hiyo ni kutokana na maandalizi ya kutosha niliyoyafanya kuhakikisha tunauchukua ubingwa wa ligi kuu,” alisema Omog.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Ndanda FC, Joseph Lazaro, naye alitamba kuwa usajili na maandalizi ya timu yake yanatosha kabisa.
“Simba hatuwaogopi, bali tunawaheshimu kutokana na ukongwe wao zaidi yetu, hivyo sisi tutaingia uwanjani kwa ajili ya ushindi, ninaamini usajili tulioufanya umekidhi vigezo,” alisema Lazaro.

2 Comments
  1. [email protected] says

    narudia tena kusema nafikiri mnanipata sana wana simba msimu ulioisha niliwaambia kuwa hamtalipata kombe kuwa nafasi za juu si kuwa eti mtakuwa bingwa mwaka huu. hizo ni nguvu za soda tu, sasa subirini muone jinsi yanga itakavyo tandaza kabumbu la nguvu ikirudi kutoka kukipiga na tp mazembe, ndipo mtakapouona moto wetu. hatuwaogopi nyie ni kama kichochoro tu. narudia tena bado nyinyi ni wa hapa hapa tu, msimu uliopita mlisema mtachukua makombe yote kiliwapata nini? acheni mbwebwe zitawatokea puani. na kocha wenu omong mtamuona mwiba unaochoma hadi rohoni nakwambieni, labda siyo mimi ninayetamka haya. hebu kumbukeni coment yangu niliyotoa ndipo mtakapo nyamaza hiyo midomo yenu. subirini vipigo msambaratike kiaina. ligi bado mbichi lakini mnachoonga sana. Yanga mwendo mdundo yanga mbele kwa mbele.

  2. [email protected] says

    mnatakiwa kutulia msije kusambaratika mapema na kumuona omong si lolote maana huwa hamchelewi nyinyi kufukuza makocha wenu. sasa subirini vipigo vitakatifu mtakavyovipata na msiamini linalowatokea. eti mmefanya usajiri mzuri waapi nawaambia mmeambulia ziro distence. mtaona kampa tena kampa tena inavyotandazwa. yanga baba lao tena msimu huu. mungu yu mwema kwetu.

Leave A Reply