The House of Favourite Newspapers

Odemba Aangua Kilio Dar

Miriam Odemba

IMELDA MTEMA| IJUMAA WIKIENDA| HABARI

DAR ES SALAAM: Mwanamitindo wa kimataifa ambaye ni mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la Miss Earth 2008, Miriam Odemba amejikuta akiangua kilio baada ya kupoteza pasi yake ya kusafiria (passport) na kadi ambayo ni kibali maalum cha kuishi na kufanya kazi jijini Paris nchini Ufaransa anakoishi na kufanyia kazi zake za mitindo.

Miriam Odemba

Akizungumza na Wikienda kwa uchungu wikiendi iliyopita, Odemba alisema kuwa alikutwa na mkasa huo katika misele

yake sehemu mbalimbali jijini Dar baada ya kutua nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Alisema: “Unajua ninachojua mimi Watanzania ni wakarimu sana maana vitu kama hivyo, kama nimesahau sehemu au nimedondosha ni vizuri mtu angenipa kwa sababu ninajulikana,” alisema Odemba.

Miriam Odemba

Odemba aliongeza kuwa, anaamini kabisa kama mtu aliyeviokota au aliyevichukua angemrudishia, asingeacha kumpa asante yake lakini watu wanapenda vitu vikubwa, jambo ambalo siyo uungwana,” alisema Odemba bila kuwa na kumbukumbu za mahali alipovidondoshea au kupoteza.

 

Comments are closed.