The House of Favourite Newspapers

Onyango Atajwa Kukosa Furaha Sababu ya Kupigwa Benchi

0
Onyango hana furaha ndani ya kikosi cha msimbazi

BEKI anayekipiga katika timu ya Simba Sc, Joash Onyango kutoka nchini Kenya ametajwa kutokuwa na furaha baada ya Kocha Zorani Maki kumpiga benchi katika mechi mbili za Ligi kuu Tanzania Bara.

 

Onyango amekosa furaha kiasi cha kutaka kuvunja mkataba baada ya kocha huyo kumuweka benchi na kuwatumia mabeki wengine katika mechi mbili za ligi kuu Tanzania Bara zilizochezwa hadi sasa.

 

 

Katika kumjibu beki huyo Zorani maki alimwambia beki huyo kuwa lengo lake sio kumtenga bali ni kutengeneza muunganiko mzuri kwa kila safu, amesema kuwa Joash Onyango na Inonga tayari wameshakuwa na muungaaniko mzuri hivyo anatengeneza kombinesheni nyingine.

 

Joash Onyango

Amesema ili kuhakikisha timu inakuwa vizuri atampa nafasi kila mnchezaji hivyo ameanza na Quattra anayeonekana kuwa mtulivu katika mechi aliyocheza.

 

“Timu inapata matokeo mazuri, lakini bado tuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunakuwa imara zaidi kwa kila Idara na kuwa na muunganiko mzuri”alisema kocha huyo.

 

Katika mechi hizo mbili zilizopigwa Simba iliibuka na ushindi mnono wa wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold na mabao 2-0 dhidi ya kagera Sugar, mechi zote mbili zikichezwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa kimitandao.

Leave A Reply