The House of Favourite Newspapers

Oprah Asumbuliwa na Ugonjwa Hatari

MTANGAZAJI maarufu nchini Marekani, Oprah Winfrey, amekiri kusumbuliwa na ugonjwa hatari unaotishia maisha yake, ugonjwa ambao haupewi kipaumbele na mamia ya watu.

 

Oprah amefunguka hayo kwenye shoo ya rafiki na jirani yake wa zamani, Ellen DeGeneres, na kuusisitizia umati uliojitokeza siku hiyo kuwa ugonjwa wa Pneumonia (nimonia) ni hatari na unaua.

 

“Nilitoka safarini na nilipofika nyumbani nilijihisi nna homa…kabla yakwenda hospitali na kugundulika nna Pnemonia”, alisema Winfrey.

 

Hata hivyo,  aliongeza kuwa baada ya kulijua hilo aliendelea na kazi na kusahau kuishughulikia afya yake mpaka alipozidiwa na kupelekwa hospitali na kugundulika ugonjwa huo umefika hatua mbaya.

 

“Niliendelea na kazi na kutumia tu dawa za kupunguza maumivu hadi nilipozidiwa na kupelekwa kwa mtaalam wa mapafu aliyenihudumia mpaka nikapona, ila aligundua ugonjwa umefikia pabaya na akaniomba niahirishe mipango yangu yote ya kazi kwa mwezi mmoja ili kuokoa uhai wangu”, alieleza mtangazaji huyo.

 

Oprah kwa sasa anaanda ziara maalum kwa ajili ya kutoa elimu juu ya hatari ya ugonjwa huo.

Comments are closed.