The House of Favourite Newspapers

Pacquiao astaafu baada ya kumtwanga Bradley

0

imothy-Bradley-falls-after-he-is-hit-by-Manny-Pacquiao Timothy Bradley akianguka chini baada ya kupigwa ngumi na Mann Pacquiao

Manny-Pacquiao-gestures-to-fans-as-he-celebrates-after-defeating-Timothy-Bradley-Jr

Manny Pacquiao akishangilia ushindi baada ya kumpiga Timothy Bradley

Manny-Pacquiao-gestures-to-fans-celebrating-after-defeating-Timothy-Bradley-JrManny Pacquiao akishangilia ushindi

Manny-Pacquiao-lands-a-punch-against-Timothy-Bradley

Manny Pacquiao akitupa konde kwa Timothy Bradley

Manny-Pacquiao-lands-a-punch-to-bring-down-Timothy-Bradley

Manny Pacquiao akirusha ngumi iliyomdondosha Timothy Bradley

Manny-Pacquiao-reacts-following-his-victory-against-Timothy-Bradley

Manny Pacquiao akishangilia baada ya kushinda pambano lake na Timothy Bradley

Referee-Tony-Weeks-counts-as-Timothy-Bradley-gets-up

Refaree Tony Weeks akimwesabia dakika Timothy Bradley baada ya kuangushwa na Manny Pacquiao

Referee-Tony-Weeks-counts-to-Timothy-Bradley

Refaree Tony Weeks akimwesabia dakika Timothy Bradley baada ya kuangushwa na Manny Pacquiao

Timothy-Bradley-falls-after-he-is-hit-by-Manny-Pacquiao

Timothy Bradley akianguka baada ya kupigwa ngumi nzito na Manny Pacquiao

Timothy-Bradley-moves-in-to-land-a-punch-against-Manny-Pacquiao

Timothy Bradley akirudisha mashambulizi kwa Manny Pacquiao

Timothy-Bradley-reacts-following-his-fight-against-Manny-Pacquiao

Timothy Bradley akiulizwa maswali na waadishi wa habari baada ya pambana lake na Manny Paquiao

BONDIA Manny Paquiao jana alihitimisha mchezo wa ndondi za kulipwa kwa kustaafu baada ya kumtwanga Timothy Bradley katika ukumbi wa MGM Grand huko Las Vegas, Marekani.

Mpiganaji huyo maarufu wa Kifilipino aliyeahidi kustaafu baada ya mchezo huo,  alionyesha mchezo mahiri kuliko yote katika miaka ya karibuni alimpomwangusha Bradley mara mbili ambapo mwishoni alipata ushindi wa alama 116 dhidi ya 110.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 aliyeshindwa na Floyd Mayweather katika pambano lililofanyika mwezi Mei mwaka jana, alionyesha nguvu kubwa aliporusha makonde mfululizo dhidi ya adui yake na kumfanya aonekana kuchanganyikiwa kidogo.

Mwanzoni mwa pambano hilo, Bradley alianza vizuri kwa kupata alama nyingi ambapo alionyesha ujuzi mkubwa.  Hata hivyo, pambano lilibadilika katika duru la saba ambapo Pacquiao aliyeonekana kujiamini, alirusha konde ambalo lilimpeleka Bradely chini.

Pacquiao alimwangusha tena mpinzani wake  duru mbili baadaye, hali ambayo ilimpa jukumu kubwa Bradley katika juhudi zake za kuwania ushindi.  Bradley mwenye umri wa miaka 32 na anayetumia zaidi mkono wa kulia, alionyesha jitihada ya kutaka kumtoa mpinzani wake kwa ‘knockout’, lakini Pacquiao alitumia ujuzi na ujanja wake kukwepa tishio la mfululizo wa makonde kutoka kwa mpinzani wake.

Kengele ya mwisho ilipolia, ilikuwa ni wazi kwa wapiganaji wote hao wawili na watazamaji kwamba Pacquiao alikuwa ndiye mshindi na hiyo ikawa ishara njema kwake kwa ajili ya kuachana na masumbwi kama alivyokuwa ameahidi.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

 

Leave A Reply