The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Pam D Afiwa na Baba Yake

pam-d
  Shedrack Nyato enzi za uhai wake.

Staa wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amefiwa na baba yake, Shedrack Nyato nyumbani kwake Mbagala jijini Dar jana.

Mtandao huu ukiongea na dada wa Pam D aitwaye Rehema Nyato, amesema chanzo cha kifo cha baba yao ni ugonjwa wa pumu uliomchukua muda mrefu.

pam-d-1

Staa wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’.

Msiba upo nyumbani kwake Mbagala na kesho watamsafirisha marehemu kwenda mkoani Njombe kwa mazishi.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!

 

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.