The House of Favourite Newspapers

Papa Misifa atolewa nduki Kaburu Records

0

Papaa MisifaNa Hamida Hassan

Promota maarufu, Msafiri Peter ‘Papaa Misifa’ amefukuzwa Kaburu Records na wakurugenzi wa kampuni hiyo ya Kaburu Entertainment ambao sasa wameweka uongozi mwingine.

Mmoja wa mabosi wa kampuni hiyo, Joseph Kaburu aliiambia Ebwana Dah kuwa, wameamua kumuengua Papaa Misifa baada ya kuleta mizinguo na sasa wanajipanga kuweka mtu mwingine atakayefanya kile wanachokitaka.

“Papaa Misifa alitaka kuihujumu studio yetu baada ya kumpa mamlaka, tumeamua kumuondoa na kazi zinaendelea kama kawaida hivyo msanii mwenye kipaji aje, tutafanya naye kazi,” alisema Joseph.

Papaa Misifa alipotafutwa na safu hii kuzungumzia kile kilichompata alisema, ataandaa mkutano rasmi kueleza hatua atakazochukua.

 

Leave A Reply